Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 42 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 497 | 2026-06-03 |
Name
Benjamin Lukubha Ngayiwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kahama Mjini
Primary Question
MHE. BENJAMIN L. NGAYIWA aliuliza: -
Je, lini barabara za ndani katika Jimbo la Kahama Mjini zitajengwa kwa kiwango cha lami na changarawe ili kuepuka adha ya usafiri?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Benjamin Lukubha Ngayiwa, Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kutekeleza mpango wa ujenzi wa barabara katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama. Kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri ya Manispaa ya Kahama imetenga kiasi cha shilingi milioni 600 na mwaka 2026/2027 kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilometa moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali ina mpango wa kujenga kwa kiwango cha changarawe barabara zenye urefu wa kilometa 51.43 kwa gharama ya shilingi milioni 716.95. Vilevile, katika mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali imepanga kujenga barabara za ndani zenye urefu wa kilometa 58.5 kwa kiwango cha changarawe kwa gharama ya shilingi milioni 767.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya uboreshaji wa barabara za ndani na Manispaa ya Kahama kwa kiwango cha lami na kiwango cha changarawe ili ziweze kupitika wakati wote. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved