Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Benjamin Lukubha Ngayiwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kahama Mjini
Primary Question
MHE. BENJAMIN L. NGAYIWA aliuliza: - Je, lini barabara za ndani katika Jimbo la Kahama Mjini zitajengwa kwa kiwango cha lami na changarawe ili kuepuka adha ya usafiri?
Supplementary Question 1
MHE. BENJAMIN L. NGAYIWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali lakini nipende tu kuweka swali la nyongeza kwamba Mji wetu wa Kahama umekuwa ni mji ambao unakuwa na changamoto kubwa sana ya kupitika kwa barabara hasa wakati wa masika, Kata ya Majengo, Kata ya Mhungula, Malunga, Nyahanga, Nyasubi, Mhungula na hasa ile barabara ya kuelekea kwenye machimbo kule Mwine ambayo inaingiza fedha nyingi sana Serikalini bado zinakuwa hazipitiki wakati wa mvua.
Sasa nini mpango wa Serikali kwenda kuongeza bajeti ya ujenzi wa barabara za lami kutoka kilometa moja kwa kila mwaka twende kilometa tatu kwa kila mwaka? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza, nimpongeze sana Mheshimiwa Benjamin Lukubha Ngayiwa, Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini kwa namna ambavyo amekuwa mwakilishi madhubuti sana wa wananchi wa Jimbo la Kahama Mjini, na mimi nimhakikishie kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI tutahakikisha tunampa ushirikiano wa kutosha ili barabara za Jimbo la Kahama Mjini ziweze kupitika vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika majimbo na manispaa ambazo zimetengewa fedha nyingi kwa ajili ya uboreshaji wa barabara za changarawe na lami Jimbo la Kahama Mjini ni moja ya majimbo hayo. Kwa mfano, kupitia Mradi wa TACTIC hivi sasa ambao tayari tumeshasaini mkataba na kazi zinaanza kuendelea tayari tumetenga shilingi bilioni 22.31 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami Kahama Mjini, kilometa 16.58 ambazo zitajengwa katika maeneo ya eneo la mjini kilometa 12.13, eneo la viwanda Zongomera kilometa 3.08, eneo la kituo cha mabasi na soko kilometa 1.37. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama haitoshi katika bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 tumetenga shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami kilometa moja, lakini pia tumetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za changarawe zaidi ya kilometa 58.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imedhamiria kuhakikisha kwamba Manispaa ya Kahama inakuwa na barabara bora za lami na changarawe na tutaendelea kutenga fedha ili ziweze kujengwa na kuwa na huduma nzuri ya usafiri katika Jimbo la Kahama Mjini.
Name
Bazilio Kapunda Mbwilo
Sex
Male
Party
ACT
Constituent
Nkasi Kaskazini
Primary Question
MHE. BENJAMIN L. NGAYIWA aliuliza: - Je, lini barabara za ndani katika Jimbo la Kahama Mjini zitajengwa kwa kiwango cha lami na changarawe ili kuepuka adha ya usafiri?
Supplementary Question 2
MHE. BAZILIO K. MBWILO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na neema ya mvua ambayo Wilaya yangu ya Nkasi imepata katika msimu huu imepelekea barabara zote za pale Mjini Namanyere kuharibika sana. Sasa mvua imeisha; je, ni lini Serikali itatuwezesha kujenga hizo barabara zilizoharibika vibaya? Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini kwa ufuatiliaji wake wa mara kwa mara alishakuja Ofisi za Waziri Mkuu, TAMISEMI mara kadhaa na tumemhakikisha Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatambua kufuatia mvua hizi nyingi barabara zetu zimaharibika za Jimbo la Nkasi Kaskazini, Wilaya ya Nkasi kwa ujumla lakini pia katika eneo la Namanyere.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie kwamba tayari Serikali tumeshatoa maelekezo kwa Mameneja wote wa TARURA kote nchini, TARURA Mkoa na TARURA Wilaya wanaendelea na utangazaji wa zabuni wa 60% ya bajeti kwa ajili ya matengenezo ya haraka na ya dharura kwa barabara zote zilizoathirika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nitumie nafasi hii kumsisitiza Meneja wa TARURA wa Mkoa wa Rukwa na Wilaya ya Nkasi kuongeza speed na kufika pia Namanyere na kuona barabara zilizoharibika ili ziweze kupata kipaumbele kwenye bajeti ambayo tayari tumetangaza kwa ajili ya kupata wakandarasi.
Name
Dr. Lazaro Killiani Komba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Peramiho
Primary Question
MHE. BENJAMIN L. NGAYIWA aliuliza: - Je, lini barabara za ndani katika Jimbo la Kahama Mjini zitajengwa kwa kiwango cha lami na changarawe ili kuepuka adha ya usafiri?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. LAZARO K. KOMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ili nami nipate kuuliza swali la nyongeza kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Peramiho. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya kutoka Songea Mjini kupitia Liwena, Kijiji cha Lipaya hadi kufika Mpitimbi ambapo inaunganika na barabara ile ya Likuyufusi - Mkenda ni barabara ya miaka mingi sana, na barabara hii haijafanyiwa ukarabati kwa muda mrefu na sasa tunavyozungumza daraja linalounganisha vijiji hivi limekwishaanza kukatika.
Je, ni lini sasa Serikali itaijenga barabara hii kwa kiwango cha lami? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nimpongeze sana Mheshimiwa Dkt. Komba, Mbunge wa Jimbo la Peramiho kwa ufuatiliaji wake wa mara kwa mara na nitumie nafasi hii kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Peramiho kwamba kipaumbele cha Serikali kwenye miradi ya barabara ni kuhakikisha maeneo yote korofi yanajengwa ili wananchi waweze kusafiri na kusafirisha bidhaa zao bila kikwazo vyovyote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo nitumie nafasi hii nimwelekeze Meneja wa TARURA wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na Meneja wa TARURA Wilaya ya Songea wafike kwenye barabara hii ambayo Mheshimiwa Mbunge ameitaja kutoka Songea kwenda maeneo mengine ili waifanyie tathmini. Kwanza, wajiridhishe na hali ya daraja hilo kama linaweza likafanyiwa matengenezo kabla halijaharibika, tuweze kufanya matengenezo ya dharura ili daraja hilo lisikatike, lakini tuone gharama zinazohitajika kwa ajili ya matengenezo ya barabara hiyo ambayo haijatengenezwa muda mrefu ili Serikali iweze kutenga bajeti kwa ajili ya matengenezo ya barabara hiyo.
Name
Emmanuel Peter Cherehani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ushetu
Primary Question
MHE. BENJAMIN L. NGAYIWA aliuliza: - Je, lini barabara za ndani katika Jimbo la Kahama Mjini zitajengwa kwa kiwango cha lami na changarawe ili kuepuka adha ya usafiri?
Supplementary Question 4
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Barabara inayotoka Kata ya Nyankende inapita Nyambeshi, Kata ya Bulungwa, Sabasabini, Kata ya Mpunze inayotuunganisha na Manispaa ya Kahama haipitiki kabisa na ndio inayolinda uchumi wa Halmashauri ya Ushetu.
Ni nini mkakati wa Serikali kuifanyia marekebisho ya dharura hiyo barabara? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba ziko barabara nyingi ambazo zimeathirika na mvua nyingi zilizonyesha msimu ulipita na tayari mkakati wa Serikali umeanza kutekelezwa ambao ni kutangaza zabuni, kupata wakandarasi kwa ajili ya kufanya matengenezo ya barabara zote zilizokatika na kuharibika zile barabara muhimu sana ambazo ni uti wa mgongo wa maeneo husika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo barabara hiyo inaunganisha Ushetu na Kahama ni barabara muhimu na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tayari Meneja wa TARURA wa Shinyanga lakini pia wa Wilaya ya Kahama na Ushetu wameshatangaza zabuni, tutapata wakandarasi hivi karibuni kwa ajili ya kufanya marekebisho kwenye barabara hizo. (Makofi)
Name
Zuberi Yahya Mfaume
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Morogoro Kusini
Primary Question
MHE. BENJAMIN L. NGAYIWA aliuliza: - Je, lini barabara za ndani katika Jimbo la Kahama Mjini zitajengwa kwa kiwango cha lami na changarawe ili kuepuka adha ya usafiri?
Supplementary Question 5
MHE. ZUBERI Y. MFAUME: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Mimi ninatokea Jimbo la Morogoro Kusini, ningependa kujua Barabara ya Kilengezi, Kongwa hadi Lukooni lini itaanza kutengenezwa ipo kwenye hali mbaya sana? Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ziko barabara na hususani katika Jimbo la Morogoro Kusini ambalo lina neema ya mvua nyingi sana na kila msimu wa mvua barabara nyingi zinaathirika sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mheshimiwa Zuberi, kwamba Serikali inaendelea kwanza tumeshafanya tathmini ya barabara zote zilizoharibiwa na mvua na tumeshapata gharama ya fedha ambazo zinahitajika takribani shilingi bilioni 300 na hivi sasa Serikali inaendelea na taratibu za kibajeti kwa ajili kuanza kupeleka fedha kwa utaratibu wa dharura, lakini pia utaratibu wa kibajeti ili kurekebisha barabara hizo.
Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa awamu tutahakikisha tunaendelea kufanya matengenezo katika barabara hiyo.
Name
Ibrahim Mohamed Shayo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Mjini
Primary Question
MHE. BENJAMIN L. NGAYIWA aliuliza: - Je, lini barabara za ndani katika Jimbo la Kahama Mjini zitajengwa kwa kiwango cha lami na changarawe ili kuepuka adha ya usafiri?
Supplementary Question 6
MHE. IBRAHIM M. SHAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi, kuna Mradi wa TACTIC wenye gharama ya shilingi bilioni 22.9 barabara ya kilometa 13.3 ambao uko Mjini Moshi. Mradi huu mkandarasi anautengeneza kwa kusuasua sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nini kauli Serikali kuhusu mradi huu kuweza kwenda kwa wakati?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa TACTIC katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwa Mheshimiwa Mbunge Ibrahim ni moja ya miradi 45 inayotekelezwa na Serikali, na ni kweli kwamba tumekwishapata mkandarasi lakini utekelezaji au kasi ya utekelezaji wa mradi ule hairidhishi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimjulishe Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI kupitia TARURA tumekwisha mwelekeza; kwanza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, lakini na timu yetu ya wataalam ikae na mkandarasi mapema iwezekanavyo tuweze kuona nini changamoto ya mkandarasi ili tuweze kuchukua hatua ikiwemo na ikiwezekana kuvunja mkataba kwa kadri ya vifungu vya mkataba au kuhakikisha anaanza kufanya matengenezo ya barabara hiyo ili iweze kukamilika kwa mapema iwezekanavyo.
Name
Dr. Christina Christopher Mnzava
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BENJAMIN L. NGAYIWA aliuliza: - Je, lini barabara za ndani katika Jimbo la Kahama Mjini zitajengwa kwa kiwango cha lami na changarawe ili kuepuka adha ya usafiri?
Supplementary Question 7
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kunipa nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo la Solwa, Kata ya Salawi kuna center inaitwa Pango ni center ambayo ipo busy sana kwa biashara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ili uwe na taa za barabarani kufanya biashara usiku ni lazima kuwe na lami; je, ni lini mtatuwekea walau kilometa tano za lami katika Mji wa Salawi?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Serikali imeendelea kufanya tathmini ya miji yetu midogo inayoibuka na kuweka mipango ya kuiboresha miji ikiwemo utaratibu wa kupendezesha miji yetu na moja mpango huo ni kuhakikisha kwamba tunajenga angalau vipande vya barabara za lami, lakini kuweka taa za barabarani ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli zao za kiuchumi ikiwezekana hata usiku.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Dkt. Mnzava tumepokea hoja ya mji huo na tutamtuma Meneja wa TARURA, Mkoa wa Shinyanga na Meneja wa Wilaya wafanye tathmini, watuletee makadirio ya angalau kilometa chache za lami na ili tuweze kuona uwezekano wa kutenga bajeti kwa awamu kwa ajili ya kujenga barabara na kuweka taa za barabarani.
Name
John John Nchimbi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyasa
Primary Question
MHE. BENJAMIN L. NGAYIWA aliuliza: - Je, lini barabara za ndani katika Jimbo la Kahama Mjini zitajengwa kwa kiwango cha lami na changarawe ili kuepuka adha ya usafiri?
Supplementary Question 8
MHE. JOHN J. NCHIMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi hii, nilikuwa ninaomba kuuliza swali moja tu la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa uzoefu tuliokuwa nao wakandarasi wa kigeni wanapofanya kazi za ukandarasi hapa nchini mara zote kwenye mikataba yao huwa wanawekewa sehemu ya interest pale ambapo wanachelewa kulipwa, lakini wakandarasi wa Kitanzania kwenye mikataba yao ya TARURA kipengele hicho hakipo na hivyo kupelekea wengi sana wanafilisiwa na mabenki pale malipo yanapochelewa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nini mpango wa Serikali wa kulinda wazawa ili waweze kukua na wenyewe wakawa na nguvu kama wakandarasi wa nje wanaolindwa na Serikali yetu? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mheshimiwa John John Nchimbi amekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa masilahi ya wakandarasi wa ndani ya nchi na mimi nimhakikishie kwamba hicho ni moja kipaumbele cha Serikali, kwanza kuhakikisha kwamba wakandarasi wa ndani ya nchi wanapata miradi na kiwango cha miradi wanayopata kilipandishwa mpaka shilingi bilioni 50, wakandarasi wazawa wanaweza kupata miradi hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu zipo changamoto za kisheria za hapa na pale ambazo ni utaratibu wa kuendelea kuziboresha kwa kadri ambavyo tunazi-experience katika utekelezaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nichukue observation Mheshimiwa Mbunge ya kuhusiana na kifungu cha penalty kwa wale wakandarasi wa nje na wa ndani na Serikali itaendelea kufanya tathmini na kuona uwezekano wa kufanya maboresho ili kuweka mazingira na uwanja mzuri kwa wakandarasi wa ndani kupata tija na faida katika miradi ya maendeleo.