Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 42 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 498 | 2026-06-03 |
Name
Mwamengo Ulimboka Baraka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyela
Primary Question
MHE. SUMA I. FYANDOMO K.n.y. MHE. BARAKA A. U. MWAMENGO aliuliza: -
Je, lini Serikali itapeleka gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya Ipinda?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Baraka Ulimboka Mwamengo, Mbunge wa Jimbo la Kyela.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua uhitaji mkubwa wa magari ya kubebea wagonjwa. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 hadi sasa Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI imepokea jumla ya magari ya kubeba wagonjwa 382 na magari 212 ya uratibu na usimamizi wa shughuli za afya. Magari hayo yamepelekwa kwenye mikoa na halmashauri zote nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Kyela ilipokea gari moja la uratibu na usimamizi wa shughuli za afya na magari mawili ya kubebea wagonjwa ambapo gari moja lipo Kituo cha Afya Kilasilo na lingine Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyela. Kwa sasa Kituo cha afya Ipinda kinahudumiwa na gari la wagonjwa lililopo Hospitali ya Wilaya ya Kyela.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili kuendelea kununua magari ya kubebea wagonjwa na kuyapeleka kwenye halmashauri zenye upungufu ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Kyela.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved