Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Suma Ikenda Fyandomo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUMA I. FYANDOMO K.n.y. MHE. BARAKA A. U. MWAMENGO aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya Ipinda?

Supplementary Question 1

MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali na sisi tunaona juhudi ya Serikali namna ambavyo inajali wananchi hasa pale wanapokuwa wanaumwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali; Wilaya ya Kyela ina upungufu wa madaktari, lakini pia hata ma-nurse. Ni lini Serikali italeta madaktari wa kutosheleza Wilaya ya Kyela?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na swali hilo, mimi kama Mbunge wa Mkoa wa Mbeya wa Viti Maalum hilo tatizo lipo hata Wilaya ya Mbarali, Chunya, Rungwe, Mbeya DC lakini pia lipo pamoja na Kyela yenyewe. (Makofi)

Sasa je, ni lini Serikali itatoa tatizo hilo lote kwa ujumla wake ili wananchi wanapokuwa wanaumwa wapate huduma kwa haraka?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge na ameongea kwa niaba ya mkoa kwa sababu ni Mbunge wa mkoa anafahamu changamoto za mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuajiri madaktari na mwaka wa fedha uliopita ambapo Mheshimiwa Rais aliridhia vibali 5,000 vya madaktari na wataalam wetu wa afya (wauguzi) na tukawasambaza kwenye halmashauri zote nchini na kwa wastani kila halmashauri ilipata angalau wataalam 100 mpaka 200 ili waende wakatoe huduma ambazo Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaahidi wapiga kura wetu, wananchi wa Tanzania kwenye kampeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi tutaendelea kutekeleza ahadi ambazo Mheshimiwa Rais ambazo amezitoa kwenye kampeni kuhakikisha tunapeleka madaktari wataalam ili waende wakatoe huduma zetu na kupunguza referral ambazo sio za lazima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge wa Mkoa kwamba tutaendelea kutenga wataalamu wetu na kuwapeleka katika maeneo hayo ili waende wakatoe huduma hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.

Name

Moshi Selemani Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tanganyika

Primary Question

MHE. SUMA I. FYANDOMO K.n.y. MHE. BARAKA A. U. MWAMENGO aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya Ipinda?

Supplementary Question 2

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Tarafa ya Mwese na Kituo cha Afya cha Mwese, Katuma hakina gari ya kubebea wagonjwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini Serikali itapeleka gari kwenye tarafa hiyo ili kuokoa wananchi ambao wanapata shida na adha kwenye vituo hivyo vya afya?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kakoso.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kupeleka magari kwenye halmashauri zetu hasa zile ambazo zina upungufu mkubwa wa magari na awamu hii inayofuatia tutaendelea kupeleka magari hasa kwenye zile halmashauri ambazo hazikupata kwa awamu iliyopita ili kuona namna gani zinaendelea kutoa huduma kwa mama zetu hasa wale wajawazito.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tunaendelea kutoa taarifa na tunaendelea kuwapa wakurugenzi wetu lakini pia ma-DMO kuendelea kutumia ile huduma ya M-Mama ambayo Serikali inashirikiana na Vodacom kuhakikisha kwamba unaweza ukapata gari binafsi na likaenda likabeba ugonjwa wetu hasa kutoka ngazi ya afya ya msingi au katika kaya na kuwapeleka katika vituo vyetu vya afya na halmashauri zimekuwa zikilipa magari hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nikuhakikishie kwamba tutaendelea kuangalia upungufu hasa katika maeneo ya halmashauri ambazo zina upungufu wa magari na kuziongezea magari hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.

Name

Sara Msafiri Ally

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mvomero

Primary Question

MHE. SUMA I. FYANDOMO K.n.y. MHE. BARAKA A. U. MWAMENGO aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya Ipinda?

Supplementary Question 3

MHE. SARA M. ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Kwanza ninaishukuru sana Serikali kwa kutupa gari la wagonjwa kwenye Kituo cha Afya cha Mziha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na changamoto za kijiografia kwenye Jimbo la Mvomero bado tunahitaji Serikali itusaidie kuleta gari la wagonjwa kwenye Kituo cha Afya cha Mlali, Mgeta na Kibati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, lini Serikali italeta magari hayo ili kusaidia huduma hii ya afya iweze kufanya vizuri kwa wananchi wa Mvomero?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge wa Mvomero na tulifanya ziara ile siku ya Muungano katika jimbo lake na wananchi wanampenda kweli kweli kwa sababu ikitokeza kwa wingi ili kushuhudia ile ziara na kutupa moyo watendaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutaendelea kutenga bajeti ya kuongeza magari kadri ambavyo tunayapata kutoka Wizara ya Afya ili kuona namna gani tunaendelea kuwasaidia mama zetu, wagonjwa katika Jimbo la Mvomero.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge nimhakikishie ushirikiano kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kadiri ambavyo tunapokea magari na sisi tutaelekeza hasa kwenye halmashauri ambazo zina upungufu mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.

Name

Adonis Alfred Bitegeko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba Kaskazini

Primary Question

MHE. SUMA I. FYANDOMO K.n.y. MHE. BARAKA A. U. MWAMENGO aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya Ipinda?

Supplementary Question 4

MHE. ADONIS A. BITEGEKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru kwamba Wilaya ya Muleba Serikali imejenga hospitali ya wilaya, lakini pia katika Jimbo la Muleba Kaskazini Serikali imejenga Kituo cha Afya cha Izigo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vituo hivyo vya kutoa huduma za afya havina magari ya kubeba wagonjwa. Je, ni lini Serikali itapeleka nagari ya kubebea wagonjwa katika vituo hivyo vya kutoa huduma ya afya?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Muleba Kaskazini kama alivyoliuliza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaifahamu jiografia ya Mkoa wa Kagera na mimi nimepata kusoma kule, kwa hiyo, nafahamu mazingira yalivyo. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutaendelea kutenga bajeti kuangalia magari haya kadri tunavyoyapokea ili tuyaelekeze katika halmashauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa zaidi ni kuendelea kuboresha miundombinu na kupeleka wataalam madaktari katika hospitali zetu hizo na hasa ule ujenzi wa hizi maternity complex za kisasa ili zile huduma ambazo zinahitaji referral ziweze kutibiwa katika vituo vyetu na waweze kupata huduma hizo ili wasihitaji zaidi haya magari ya ambulance.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwenye maeneo yale ambayo hawana huduma kabisa tutaelekeza magari yetu haya ya ambulance kadri tunavyo yapokea ili yaende kutoa huduma kwa watu wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.

Name

Azza Hilal Hamad

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUMA I. FYANDOMO K.n.y. MHE. BARAKA A. U. MWAMENGO aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya Ipinda?

Supplementary Question 5

MHE. AZZA H. HAMAD: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Kituo cha Afya cha Tinde kilichopo Jimbo la Itwangi kiko barabara kuu na kinahudumia kata 10 ndani ya tarafa moja na watu mbalimbali wanaotoka maeneo tofauti kwa sababu ya maeneo kilichopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Tinde lilipata ajali mbaya sana zaidi ya miaka mitano sasa na halijaweza kutengenezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itatuletea gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Tinde?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Azza, Mbunge wa Jimbo la Itwangi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kweli Jimbo la Itwangi lina kata 14 na lina upungufu wa vituo vya afya, kwa hiyo, tukipelekea Mheshimiwa Mbunge gari la ambulance angalau wataweza kusaidia zile kata ambazo hazina vituo vya afya ili kuwahisha wagonjwa wetu katika Kituo cha Afya cha Tinde na kituo hiki kiko barabarani kwa hiyo kuna muda ambao tunapata zile ajali na wanahitaji msaada wa ambulance.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa Serikali tunafahamu changamoto hiyo, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI tunaenda kukupa ushirikiano Mheshimiwa Mbunge kuhakikisha kwamba tunapeleka gari la wagonjwa hili liende kusaidia wagonjwa wetu katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.

Name

Issa Ally Mchungahela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lulindi

Primary Question

MHE. SUMA I. FYANDOMO K.n.y. MHE. BARAKA A. U. MWAMENGO aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya Ipinda?

Supplementary Question 6

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, katika Jimbo la Lulindi kwenye Kata ya Mkululu na Kata ya Namwanga kuna vituo vya afya ambavyo vinahudumia maeneo makubwa sana katika jimbo hilo, lakini havina magari ya wagonjwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini mtapeleka magari ya wagonjwa katika vituo hivyo viwili?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nilijibu kwenye swali la msingi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge Mchungahela kwamba tutaendelea kupeleka magari kwenye halmashauri hasa zile ambazo zina upungufu mkubwa na zipo pembezoni zaidi na zina uhaba mkubwa wa wataalam wetu ili kuhakikisha kwamba wagonjwa wetu wanaohitaji huduma hizi wawahishwe katika vituo ambavyo vinatoa huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Mchungahela nikuhakikishie katika maeneo ambayo umeainisha na sisi Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI tutaendelea kupeleka magari haya ili yaende yakaokoe maisha ya wagonjwa wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.