Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 42 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 501 2026-06-03

Name

Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Primary Question

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA Wilaya Biharamulo ili kuwezesha vijana kujikwamua kutokana na mafunzo yanayotolewa?

Name

Wanu Hafidh Ameir

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ruhusa yako na kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ninaomba kujibu swali namba 501 la Mheshimiwa Engineer Ezra John Chiwelesa, Mbunge wa Biharamulo Magharibi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo cha VETA cha Wilaya ya Biharamulo ni miongoni mwa vyuo 64 vya VETA vinavyojengwa na Serikali katika Mkoa na Wilaya ambazo hazina Vyuo vya Ufundi Stadi. Mradi huu unalenga kuongeza fursa za mafunzo na kusogeza huduma karibu na wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Biharamulo unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2026. Hadi sasa Serikali imetumia kiasi cha shilingi bilioni 1.12 kati ya shilingi bilioni 1.6 zilizotengwa kwa ajili ya kukamilisha awamu ya kwanza ya mradi huu na ujenzi wake umefikia 72%.