Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Primary Question

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA Wilaya Biharamulo ili kuwezesha vijana kujikwamua kutokana na mafunzo yanayotolewa?

Supplementary Question 1

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, nina hoja tu kama mbili ambazo ninazo na mradi huu ulianza mwaka 2023. Tumefanya extension tulitegemea umalizike mwaka 2024 lakini haujamalizika mpaka sasa. Kwa hiyo, tunajua nia njema ya Serikali, lakini miradi hii ya ujenzi kwanza inakuwa na mkandarasi anayejenga mradi unapochukua muda mrefu sana, unaongeza gharama kwa mkandarasi, lakini gharama hata kwa wananchi pale kwa sababu tulitegemea mradi huo uwe umemalizika na uanze kutoa huduma kwa wananchi. Kwa mfano kunakuwa na zile performance guarantee na vitu vingine kama hivyo. Kila inapo-expire lazima mtu aende aka-renew tena maana huwezi kuendelea na mradi ukiwa nje ya performance. Sasa zote hizo ni gharama ambazo zinaongezeka, lakini tumekuwa na shida ya umeme pia pale, kwa sababu unahitajika shilingi milioni 90 ili umeme uweze kuingizwa pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilichokuwa ninaomba kujua, cash flow si nzuri, ninataka nisikie kauli ya Serikali kuhusu cash flow ili tuweze kumalizia haya majengo ambayo yameshaanza, lakini shida kubwa ni umeme. Lile eneo halina umeme kabisa na eneo ambalo tumechukua sasa stage zinazofuata nyingi hazitaendelea bila kuwa na umeme.

Kwa hiyo, nilitaka kupata kauli ya Serikali, kama tunaweza kupata shilingi milioni 90 ile kwa haraka kwanza tuingize umeme ili hatua nyingine zinazoendelea za ujenzi wa kumalizia ziweze kufanyika hali kukiwa na umeme tayari pale. Maji tulishafikisha, lakini shida ni umeme. Ninaomba kusikia kauli ya Serikali juu ya hayo, ahsante sana.

Name

Wanu Hafidh Ameir

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ezra Chiwelesa, Mbunge wa Biharamulo Magharibi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakiri kwamba ujenzi huu wa vyuo hivi umechelewa, lakini kama tulivyosema katika bajeti ya Wizara ya Elimu kwamba fedha tayari zilishatengwa na tayari zimeanza kutoka, na fedha hizi zitaingia kwa awamu kwa kila chuo. Tayari nimeanza kupokea mrejesho kutoka baadhi ya vyuo kwamba tayari fedha hizi zimeanza kuingia na wanaendelea na ujenzi. (Makofi)

Kwa hiyo, nimuahidi Mheshimiwa Ezra kwamba fedha itakuja, ujenzi utaendelea, na suala la umeme tutafuatilia pamoja mimi na yeye. (Makofi)

Name

Paschal Inyasi Chinyele

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Primary Question

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA Wilaya Biharamulo ili kuwezesha vijana kujikwamua kutokana na mafunzo yanayotolewa?

Supplementary Question 2

MHE. PASCHAL I. CHINYELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekamilisha ujenzi wa Chuo cha Ufundi (Dodoma Polytechnic College) katika Mtaa wa Lugala, Kata ya Mbalawala. Je, ni lini Serikali itaanza kuchukua wanafunzi katika chuo hicho ambacho kiko ndani ya Jiji la Dodoma?

Name

Wanu Hafidh Ameir

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Chinyele, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Serikali imekamilisha kwa kiasi fulani ujenzi wa Dodoma Polytechnic, na kama Mheshimiwa Mbunge anakumbuka vizuri tulifanya ziara pamoja katika chuo kile na hatua iliyofikia ni nzuri. Kwa hiyo, tu nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inaenda kumalizia ukamilishaji wa chuo kile na matarajio ya mafunzo ni kuanza mwaka huu wa 2026/2027. (Makofi)

Name

Kunti Yusuph Majala

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA Wilaya Biharamulo ili kuwezesha vijana kujikwamua kutokana na mafunzo yanayotolewa?

Supplementary Question 3

MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kuniona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuishukuru sana Serikali, tumshukuru Dkt. Samia kwa kutupatia chuo kizuri na watoto wetu kuendelea kupata ujuzi na kujiongezea ajira kwenye maeneo yao, lakini Mheshimiwa Naibu Waziri, ulifika Chuo cha VETA Chemba. Tunakushukuru sana, tulikupa kilio chetu, ujenzi wa fence tunakushukuru umetupatia shilingi milioni 100, fence yetu imeanza. Ni lini sasa changamoto yetu ya pili ya uongezaji wa walimu kwenye chuo kile ili watoto wetu waendelee kunufaika na uwepo wa chuo hicho ndani ya Wilaya yetu ya Chemba?

Name

Wanu Hafidh Ameir

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kunti Majala, Mbunge wa Chemba kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Mheshimiwa Majala alifikisha changamoto hizi mbili na ile moja tayari imeanza kupata suluhisho, lakini nimuahidi kwamba kama vile ambavyo tume-solve hii changamoto ya kwanza, basi tunaenda kumalizia hii changamoto nyingine. Kwa hiyo, asiwe na wasiwasi, kati ya Vyuo vya VETA ambavyo vimepata bahati kimoja ni Chuo cha VETA Chemba. Kwa hiyo asiwe na wasiwasi, changamoto yake tunaenda kuimaliza. (Makofi)