Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 23 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 253 | 2026-05-06 |
Name
Emmanuel John Khambay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Mjini
Primary Question
MHE. EMMANUEL J. KHAMBAY aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga Barabara kilometa 24 kutoka Kona ya Mrara hadi Lango la Hifadhi ya Tarangire kwa upande wa Kijiji cha Mamire kwa kiwango cha lami?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Emmanuel John Khambay, Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa ujenzi wa barabara ya kutoka kona ya Mrara hadi Lango la hifadhi Tarangire kwa upande wa Kijiji cha Mamire yenye urefu wa kilometa 24 kwa kiwango cha lami ambayo itachochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wanaopitiwa na barabara hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2025/2026, Serikali imeanza uboreshaji wa barabara hii yenye urefu wa kilometa 24 kwa kufanya usanifu wa kilometa 0.8 na kujenga kwa tabaka la lami pamoja na ujenzi wa daraja la Mrara kwa gharama ya shilingi milioni 944.88 ambapo mkandarasi amepatikana ili kuanza ujenzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea na ujenzi wa barabara hii kwa tabaka la lami pamoja na ujenzi na matengenezo ya Barabara za Jimbo la Babati Mjini kwa kutenga bajeti kwa awamu, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved