Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 23 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 254 | 2026-05-06 |
Name
Ester Amos Bulaya
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza kutekeleza Mradi wa TACTIC unaopaswa kujengwa Jimbo la Bunda Mjini?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Ester Amos Bulaya, Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Mji wa Bunda ni miongoni mwa Miji 45 inayotekeleza Mradi wa TACTIC nchini. Mji wa Bunda upo kundi la Tatu la utekelezaji lenye Miji 18.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa TACTIC umekamilisha usanifu wa miradi ya kundi hili la tatu ikiwemo Mji wa Bunda wenye Barabara nane zitakazojengwa kwa lami. Jumla ya kilometa 5.21 pamoja na Ujenzi wa Stendi kuu ya mabasi, na Soko kuu katika mji wa Bunda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kukamilisha usanifu wa miradi hii, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia inaendelea na taratibu za kifedha ili kuanza utekelezaji wa miradi katika kundi hili ukiwemo mradi wa Mjini wa Bunda, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved