Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ester Amos Bulaya
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza kutekeleza Mradi wa TACTIC unaopaswa kujengwa Jimbo la Bunda Mjini?
Supplementary Question 1
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Kwanza, niipongeze Serikali kwa hii miradi ya TACTIC kwani inabadilisha miji kabisa na kwenda kuchechua uchumi kwenye maeneo husika. Sasa ningependa kujibiwa maswali yangu mawili ya nyongeza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali hili nimeuliza zaidi ya miaka minne na nilishaambiwa kila kitu kimekamilika, bado ujenzi kuanza na Bunge hili hili nimeliuliza nikaambiwa kila kitu kimekamilika ujenzi unaanza tire three. Wananchi wa Bunda wanataka kujua lini? Kwa sababu hili jibu nimeshajibiwa sana, lini mradi unaanza? Ndiyo fahari yao, na wanausubiri kwa hamu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Mwanzo kwenye huu mradi ilikuwa machinjio ya kisasa; lilikuwepo na dampo lijengwe, na hizi kilometa za lami hapa zimepungua. Mwanzo zilikuwa kilometa 21. Nini kimesababisha hivi vingine vyote vimeondolewa kwenye mradi, imebaki stendi, soko pamoja na barabara kilometa tano badala ya kilometa 21?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninafahamu kwamba Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, dada yangu Mheshimiwa Ester Bulaya angependa kuona leo hii barabara yote kilometa 25 imejengwa kwenye Jimbo la Bunda, na hiyo ndiyo dhamira ya Serikali yetu, na ndiyo dhamira ya Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ndiyo maana aliuleta mradi huu mahususi kwa miji 45 ili kuchachua Uchumi, na kuwezesha miundombinu yetu kuwa bora zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari tumetekeleza awamu ya kwanza, awamu ya pili, tuko hatua mbalimbali, lakini awamu ya tatu, tumeshafanya usanifu na tunaendelea na utaratibu wa kifedha ili kuanza utekelezaji wa mradi huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni kweli Mheshimiwa Mbunge ameuliza kwa muda mrefu, na kwa sababu ninafahamu ni dhamira ya kutaka kazi hii ifanyike mapema, Serikali iliweka mpango tangu mwanzo kuanza awamu ya kwanza, baada ya muda fulani tumekwenda awamu ya pili, baada ya muda fulani tumekuja awamu ya tatu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hatukupanga kuanza miradi hii tire three kwa pamoja. Vinginevyo tusingekuwa na sababu ya kuweka makundi matatu kama tungeanza pamoja. Kwa hiyo, makundi matatu yaliwekwa kwa sababu tunakwenda kwa awamu na kundi hili la tatu sasa la miji takribani 18 ndiyo tuko hatua za mwisho za kuanza utekelezaji wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Bunda Mjini kwamba Serikali itakwenda kutekeleza kama ilivyoweka mpango wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili, miradi hii ilifanyiwa usanifu lakini kutokana na upatikanaji wa fedha tumeendelea ku-review upana (scope) wa hii miradi kadiri muda unavyozidi kwenda ili kuwa na miradi ambayo inatekelezwa kutokana na upatikanaji wa fedha iliyopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, haimaanishi kwamba miradi hiyo mingine haitatekelezwa, tunatekeleza kwanza miradi hii kwa awamu hii kutokana na uwezo wa kifedha uliopo, lakini baada ya hapo tutaendelea Serikali ni endelevu na bajeti ni endelevu, tutandelea kutekeleza miradi hiyo. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Bulaya kwamba hata hayo maeneo mengine Serikali itaendelea kuyatekeleza kwa awamu. (Makofi)
Name
Omary Marcus Msigwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Madaba
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza kutekeleza Mradi wa TACTIC unaopaswa kujengwa Jimbo la Bunda Mjini?
Supplementary Question 2
MHE. OMARY M. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Wino - Matumbi iliyopo katika Jimbo langu la Madaba ni barabara muhimu kwa uwekezaji, lakini imekuwa ikijifunga kila wakati. Je, ni lini sasa Serikali itakwenda kuijenga kwa kiwango cha changarawe? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Msigwa amefuatilia kwa karibu sana kuhusiana na miundombinu ya barabara katika Jimbo la Madaba, nami nimhakikishie, yeye mwenyewe ameleta taarifa za uhitaji wa barabara na Meneja wake wa TARURA, ameleta na Ofisi ya Waziri Mkuu, tayari tumeanza utaratibu wa kutafuta fedha kwenda kutekeleza barabara hizo. (Makofi)
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza kutekeleza Mradi wa TACTIC unaopaswa kujengwa Jimbo la Bunda Mjini?
Supplementary Question 3
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ni lini Mradi wa TACTIC unaohusu barabara, soko na stendi ya mkoa utaanza kutekelezwa kwenye Mji wa Vwawa, ambao tumekuwa tunaahidiwa karibu zaidi ya miaka minne? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Mji wa Vwawa ni moja ya miji 45 kwenye Mradi wa TACTIC na uko awamu ya tatu yenye miji 18, na nimhakikishie tu kwamba, sasa tunaelekea kuanza utekelezaji wa awamu ya tatu ya miji 18, ikiwemo Mji wa Vwawa. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved