Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 23 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 255 | 2026-05-06 |
Name
Subira Khamis Mgalu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza utekelezaji wa Mradi wa TACTIC katika Jimbo la Bagamoyo baada ya usanifu kukamilika?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Subira Khamis Mgalu, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo ni miongoni mwa miji 45 inayotekeleza Mradi wa TACTIC nchini wenye barabara zenye urefu wa jumla ya Kilometa 4.5 pamoja na ujenzi wa barabara hizo kwa kiwango cha lami. Mradi huu pia utahusisha ujenzi wa stendi kuu ya mabasi Bagamoyo katika Kata ya Nia Njema, eneo la Kichemchem.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kukamilisha usanifu wa miradi hii, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia inaendelea na taratibu za kifedha kabla ya kuanza utekelezaji wa Miradi katika kundi hili ukiwemo Mji wa Bagamoyo.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved