Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 23 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 257 2026-05-06

Name

Fadhili Fabian Ngajilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Primary Question

MHE. FADHILI F. NGAJILO aliuliza: -

Je, lini huduma za kibingwa za magonjwa kama moyo, kansa, mapafu, figo na ini zitatolewa katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini?

Name

Dr. Florence George Samizi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali Kanda ya Mbeya na hospitali za rufaa za Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na Songwe zinatoa huduma za ubingwa katika fani za magonjwa mbalimbali ikiwemo moyo, saratani, mapafu, figo na ini. Hospitali ya Kanda ya Mbeya inatoa huduma za ubingwa bobezi katika fani za upasuaji wa moyo, upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu, matibabu ya mfumo wa chakula na ini, huduma ya mfumo wa upumuaji pamoja na huduma ya upasuaji kwa watoto wachanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuimarisha utoaji wa huduma za saratani katika kanda hii, Serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa kituo cha huduma za saratani mkoani Mbeya ambacho kitakuwa sehemu ya Taasisi ya Ocean Road. Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha wananchi kupata huduma za ubingwa za saratani katika kanda hii, hivyo kuwapunguzia gharama za kufuata huduma hizi katika Taasisi ya Saratani Ocean Road Jijini Dar es Salaam. Ninaomba kuwasilisha.