Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 23 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 259 | 2026-05-06 |
Name
Silvestry Fransis Koka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibaha Mjini
Primary Question
MHE. DKT. SELEMANI S. JAFO K.n.y. MHE. SILYVESTRY F. KOKA aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa Barabara ya TAMCO hadi Mapinga utakamilika kwa kiwango cha lami baada ya kusuasua kwa muda mrefu?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa Barabara ya TAMCO – Mapinga unatekelezwa kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza inahusisha sehemu ya kuanzia NIDA hadi Pangani, kilometa 3.8, na awamu ya pili inahusisha sehemu ya Pangani hadi Mapinga, kilometa 14.62. Ujenzi wa barabara hii unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2027. Aidha, Serikali inaahidi kuipa kipaumbele barabara hii kama sehemu ya kupunguza msongamano kwenye Barabara Kuu ya Dar es Salaam kwenda Morogoro, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved