Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Primary Question
MHE. DKT. SELEMANI S. JAFO K.n.y. MHE. SILYVESTRY F. KOKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya TAMCO hadi Mapinga utakamilika kwa kiwango cha lami baada ya kusuasua kwa muda mrefu?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. SULEMANI S. JAFO: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii ni muhimu sana, ninafahamu kandarasi pale inaendelea, lakini speed bado siyo ya kuridhisha. Je, nini mpango wa Serikali, kwa nia njema ile ile ya kumsukuma sasa mkandarasi ilimradi aweze kukamilisha ile kazi kwa lengo la kuwasaidia watu wa Bagamoyo, kwa dada yangu Mheshimiwa Subira na watu wa Kibaha?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Barabara ile inatengeneza ring road. Ukitoka upande wa Bayamoyo, pale Baobao mpaka unafika Kibaha, na kutoka Kiluvya kuja Kisarawe pale, kilometa 22.9. Nini mpango wa Serikali kuhakikisha kile kipande cha kilometa 22.9 kutoka Kiluvya Madukani mpaka Mpuyani nacho kinaanza kazi mara moja? Ahsante sana.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi kwamba, hii barabara Serikali inaipa kipaumbele sana kwa sababu ni kweli itasaidia sana kupunguza msongamano kwenye Barabara Kuu ya Dar es Salaam na Morogoro. Tunaipa kipaumbele kuhakikisha kwamba, mkandarasi analipwa aweze kukamilisha hiyo barabara, ambayo tuna hakika itakuwa ni muhimu sana kwa kupunguza foleni. Kwa hiyo, kipaumbele ni kikubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba, kama tutaiunga hiyo barabara mpaka Kisarawe itakuwa inatengeneza ring road, ambapo watu wengine wanaweza wakapita huko. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, tayari tumekamilisha usanifu wa hiyo barabara kutoka Kibaha hadi Kisarawe, kwa hiyo, tunachosubiri tu ni fedha tuweze kuanza kuijenga kwa kiwango cha lami, ahsante.
Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. SELEMANI S. JAFO K.n.y. MHE. SILYVESTRY F. KOKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya TAMCO hadi Mapinga utakamilika kwa kiwango cha lami baada ya kusuasua kwa muda mrefu?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapongeza ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Ipogoro – Idete. Barabara hii imeishia Kibaoni. Ni lini sasa kilometa 16 za kutoka Kibaoni kwenda mpaka Dabaga itamaliziwa kwa kiwango cha lami? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapokea pongezi za Mheshimiwa Ritta Kabati, Mbunge wa Kilolo, kwa niaba ya Serikali. Hasa niseme, hii ndiyo kazi nzuri ambayo Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameifanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kukamilisha hicho kipande hadi Dabaga, tutaendelea kwa sababu, tunafanya kwa awamu. Kwa hiyo, baada ya kukamilisha awamu ya pili, ni kukamilisha hicho kipande, cha kilometa kama 66, ili barabara yote iweze kuwa ya kiwango cha lami tukizingatia kwamba, uzalishaji wa huko wa mbao na matunda ni mkubwa sana, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved