Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 23 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 260 2026-05-06

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:-

Je, lini Barabara ya kutoka Old Shinyanga hadi Iselamagazi, Makao Makuu ya Halmashauri ya Shinyanga DC, itajengwa kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Old Shinyanga hadi Iselamagazi yenye urefu wa kilometa 25 ni sehemu ya Barabara ya Salawe – Solwa hadi Old Shinyanga, yenye urefu wa kilometa 80.1. Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami imekamilika. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi, ahsante.