Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, lini Barabara ya kutoka Old Shinyanga hadi Iselamagazi, Makao Makuu ya Halmashauri ya Shinyanga DC, itajengwa kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, upembuzi yakinifu umefanyika. Ni lini fedha zitapatikana?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Barabara ya Old Shinyanga kwenda Njia Panda ya Nyasamba – Mwanza imeanza kujengwa kwa kiwango cha lami. Kuna sehemu imekamilika zaidi ya miaka minne na tayari imeanza kuharibika. Nini Kauli ya Serikali kwa Mkandarasi yule, ambaye anajenga hiyo barabara na tayari imeharibika kabla haijakamilika? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa barabara ni hatua. Hatua ya kwanza, tumekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Ukifanya hivyo, maana yake ni maandalizi ya kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami. Kwa hiyo, bajeti bado hatujaitoa, tusubiri bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwa kuisanifu tu barabara hii, maana yake ni kwamba Serikali ina mpango wa kuijenga kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili kwamba barabara imetengenezwa miaka miwili imeharibika, ninaomba hili tulichukue. Pia, ninamwelekeza Meneja wa Mkoa wa Shinyanga pamoja na TANROADS Makao Makuu waweze kwenda kuiangalia barabara hiyo waweze kutoa taarifa, tatizo ni nini, ili hatua stahiki, kama kuna uzembe umefanyika, basi tuweze kuchukua hizo hatua. ahsante. (Makofi)

Name

Chacha Mwita Wambura

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita Mjini

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, lini Barabara ya kutoka Old Shinyanga hadi Iselamagazi, Makao Makuu ya Halmashauri ya Shinyanga DC, itajengwa kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 2

MHE. CHACHA M. WAMBURA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona na kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Katika Mji wa Geita tunayo Barabara inayotoka Geita mpaka Kahama, ambayo ni tegemezi kubwa sana katika uchumi wa Mji wa Geita. Mkandarasi amesaini mkataba tarehe 01 Mwezi wa 10 na mpaka sasa barabara ile imeshindwa kuanza kwa sababu tu yule mkandarasi hajalipwa advance. Sasa je, ni lini Serikali itamlipa advance yake ili aweze kuanza kutengeneza ile barabara?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya kutoka Geita hadi Kahama imeanza kujengwa na Serikali kwa kiwango cha lami, na hasa kipande cha kutoka Kahama hadi Kapola. Barabara hii tunavyoongea, mkandarasi yupo, anaendelea kuijenga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii barabara ilikuwa imegawanywa katika vipande viwili, kutoka Ilogi – Nyarugusu hadi Mtakuja – Geita, ambapo mkandarasi tayari amesaini na tunachosubiri ni kumpa advance, ili kuunga Mkoa wa Geita na Mkoa wa Shinyanga, kwa maana ya Miji ya Geita na Kahama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua hilo ndiyo eneo ambalo kwa kweli, lina uzalishaji mkubwa, na pia, ndiyo madini mengi yako hapo. Kwa hiyo, Serikali, tunaamini katika bajeti inayokuja, hiyo barabara tutaanza kuijenga kwa sababu kinachosubiriwa ni kumlipa advance mkandarasi, ambaye tayari alisaini mkataba.

MWENYEKITI: Tumekuelewa Mheshimiwa.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Name

Zainab Rashid Kawawa

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, lini Barabara ya kutoka Old Shinyanga hadi Iselamagazi, Makao Makuu ya Halmashauri ya Shinyanga DC, itajengwa kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 3

MHE. ZAINAB R. KAWAWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa hii nafasi. Ninaipongeza Serikali kwa kuanza ujenzi wa barabara ya kutoka Mnazi Mmoja mpaka Masasi. Sasa kuna hii barabara inayotoka Masasi mpaka Nachingwea, Nachingwea mpaka Liwale, kilometa 175. Pale tumeambiwa tutajengewa kilometa 75 kuanzia Liwale mpaka Kiangara. Mkandarasi amepatikana, lakini bado hajalipwa fedha na hajaanza kazi. Ni lini sasa Serikali itatoa fedha ili mkandarasi huyu aanze kazi kutoka Liwale kuelekea kiangara?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunategemea hela katika bajeti inayokuja. Tumepanga bajeti, ikipitishwa tutamlipa huyo mkandarasi advance ili aanze kujenga hiyo barabara, ahsante.

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, lini Barabara ya kutoka Old Shinyanga hadi Iselamagazi, Makao Makuu ya Halmashauri ya Shinyanga DC, itajengwa kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 4

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Makete – Mbeya, mmemlipa fedha mkandarasi na mvua imesimama, anatakiwa aanze kufanya kazi. Ni ipi Kauli ya Serikali, hususan, kutokana na mkandarasi vifaa alivyonavyo site, havitoshelezi kuifanya kazi, na Serikali haijamtembelea. Ni lini Serikali itafika na kumpa vitendea kazi?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatoa tu maelekezo kwa sababu, mkandarasi tumemlipa fedha arejee site na aanze kazi ya ujenzi wa barabara hiyo, ahsante.