Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 23 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 262 2026-05-06

Name

Asha Juma Kombo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mfenesini

Primary Question

MHE. ASHA JUMA KOMBO aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga upya Kituo cha Polisi cha Mfenesini?

Name

Mohammed Mahmoud Ayoub

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chaani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru sana Mheshimiwa Asha na ninampongeza. Hivyo kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Asha Juma Kombo, Mbunge wa Mfenesini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mpango wa kujenga kituo kipya cha Polisi Daraja ā€œCā€ katika eneo la Mfenesini, ambacho kitagharimu kiasi cha fedha shilingi 165,228,990. Fedha hizo zinatarajiwa kutengwa kwenye bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2027/2028. Ninaomba kuwasilisha.