Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Asha Juma Kombo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Mfenesini
Primary Question
MHE. ASHA JUMA KOMBO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga upya Kituo cha Polisi cha Mfenesini?
Supplementary Question 1
MHE. ASHA JUMA KOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini tuna maswali madogo mawili (a) na (b).
(a) Kwa kuwa, kiwango hiki cha fedha kinatengwa kwa mwaka wa fedha wa bajeti ujao, kwa nini Serikali isifikirie kuongeza kiwango hicho cha fedha na kutujengea Kituo cha Polisi Daraja A?
(b) Kwa kuwa, Kituo cha Polisi cha Mfenesini kina eneo kubwa na linavamiwa na wananchi, je, Serikali haioni haja ya kutenga fedha na kukizungushia uzio kituo hicho?
Name
Mohammed Mahmoud Ayoub
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chaani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru sana Mheshimiwa Asha Juma Kombo kwa kuwa karibu sana na wananchi wake, pia kuwa karibu na Watendaji wetu wa Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi Mfenesini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza kwa maswali yake mawili ya msingi ambalo swali la (a) anataka kujua kama hakuna uwezekano wa kituo hicho cha Polisi kupandishwa hadhi kwenda kwenye Daraja A.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kumfahamisha Mheshimiwa Mbunge kuwa, Kituo cha Polisi cha Mfenesini ni kituo cha Kata. Katika utaratibu wa ujenzi wa vituo vya Polisi tuna hatua tatu kwa nne. Hatua ya kwanza ni Daraja C ambacho kina uwezo wa kuwa katika Kata. Hatua ya pili ni Daraja C kinao uwezo wa kuwa katika ngazi ya Kata. Hatua ya pili, ni Daraja B kina uwezo wa kuwa katika ngazi ya Wilaya. Hatua ya tatu ni Daraja A ambacho kinakuwa katika ngazi ya Mkoa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo Jimbo lake lipo, kuna Kituo cha Polisi cha Daraja B pale Mwera ambacho kinaendelea kumaliziwa ujenzi wake. Tuna Kituo cha Daraja A kilichopo Mwembemadema kinaendelea kutumika kama Kituo cha Polisi cha Mkoa. Hivyo, katika mpangilio huo, eneo la Mfenesini kwa kuwa halijapewa hadhi ya kiutawala kipolisi kuwa ni Wilaya, maana yake litapaswa kubeba hadhi ya Daraja C.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa swali lake la pili ambalo ni la uzio katika eneo hilo, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba eneo la Jeshi la Polisi lililopo Mfenesini hadi sasa bado halijavamiwa na lipo salama. Ni eneo lililopimwa na limetolewa hati tarehe 17 Oktoba, 2021. Hati hiyo ina eneo lenye ukubwa wa square meter 5,624. Hivyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kulinda eneo hilo na kuhakikisha kuwa lipo salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, ushauri wake wa kuzungushia uzio eneo hilo tunaendelea kulichukua.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved