Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 23 Works and Transport Wizara ya Uchukuzi 263 2026-05-06

Name

Kassim Hassan Haji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanakwerekwe

Primary Question

MHE. KASSIM HASSAN HAJI aliuliza: -

Je, lini Treni ya Mwendokasi itaanzisha safari za Mchana kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam na kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma?

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Uchukuzi, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Kassim Hassan Haji, Mbunge wa Mwanakwerekwe, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania linaendelea kutoa huduma ya usafiri wa treni kila siku kwa njia ya treni Dar es Salaam hadi Dodoma. Aidha, safari za treni kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa siku ni treni nane na safari za treni kutoka Dodoma hadi Dar es salaam kwa siku ni treni nne.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upangaji wa safari za treni unaendelea kuboreshwa ambapo ukamilikaji wa mifumo ya uendeshaji utakapokuwa imefika 100%, shirika litaongeza safari za treni ili kukidhi hitaji kubwa la wateja hasa wateja wetu wanaotoka na kuelekea Zanzibar ili waweze kuunganisha na usafiri wa treni na huduma nyingine za usafiri wanapotoka au kuelekea Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaendelea kuwaomba wateja wetu kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambapo shirika linaendelea na ukamilishaji wa mifumo. Mifumo hii inatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa 2026/2027.