Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kassim Hassan Haji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanakwerekwe

Primary Question

MHE. KASSIM HASSAN HAJI aliuliza: - Je, lini Treni ya Mwendokasi itaanzisha safari za Mchana kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam na kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma?

Supplementary Question 1

MHE. KASSIM HASSAN HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ninamshukuru Naibu Waziri kwa kujibu majibu kwa ufasaha, lakini ninaomba niwape ushauri tu. Kwa kuwa treni hizi zinaondoka muda wa saa moja na nusu kupishana, kwa nini wasisogeze mbele hizi safari ikawa kama moja inaondoka saa tatu na nyingine iondoke saa saba mchana ili kuweka hawa watu wa katikati waweze kupata nafasi ya wao kusafiri?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawashauri sana Wizara waende wakaliangalie hilo, ahsante sana. (Makofi)

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimepokea.

Name

Neema William Mgaya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KASSIM HASSAN HAJI aliuliza: - Je, lini Treni ya Mwendokasi itaanzisha safari za Mchana kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam na kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma?

Supplementary Question 2

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, usafiri wa treni ni usafiri wenye bei nafuu zaidi ukilinganisha na usafiri mwingine; na kwa kuwa, Nyanda za Juu Kusini ni wakulima wazuri, wakubwa wa zao la parachichi pamoja na horticultural kwa ujumla ikiwepo Njombe, je, Serikali mmejipanga vipi kuhakikisha kwamba mnaweka mfumo wa cold room kwenye baadhi ya mabehewa ya reli ya TAZARA ili kuweza kuwasaidia wafanyabiashara hawa?

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza Mheshimiwa Neema Mgaya kwa jinsi anavyofuatilia usafiri wa reli hususan kwenye upande wa TAZARA ambao upo Nyanda za Juu Kusini na inaunganisha na nchi zetu za Kusini mwa Afrika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa kutokana na hili Shirika letu la TAZARA ambalo tulikuwa tunafahamu lilijengwa miaka ya 1970 wakati wa Mwalimu Nyerere, kipindi chote hicho lilikuwa likiendeshwa kwa uwezo wa chini. Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya maamuzi kwa kushirikiana na viongozi wenzake wa China na Zambia na sasa hivi ninavyozungumza reli hiyo inakarabatiwa upya ili ule uwezo uliojengewa wa kusafirisha mzigo wa kutosha iweze kukamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamwomba Mheshimiwa aweze kuvumilia. Ushauri wake tumeupokea ili pengine katika maboresho hayo tuweze ku-consider na hicho alichokizungumza kuweka cold room maalum kwa ajili ya kuweza kusafirisha mazao au bidhaa muhimu kwenye ukanda huo ambao ni pamoja na parachichi.