Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 23 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 265 2026-05-06

Name

Janeth Elias Mahawanga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kuanzisha au kuimarisha mifuko maalum ya uwezeshaji kwa wanawake?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Janeth Mahawanga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, inatekeleza mpango madhubuti wa kuimarisha mifuko ya uwezeshaji kiuchumi ukiwemo Mfuko Maalum wa Maendeleo ya Wanawake (Women Development Fund) ambao upo chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum. Mfuko huo unatoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wanawake wajasiriamali, iwe ni mtu mmoja mmoja au vikundi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, mkakati endelevu uliopo ni kuimarisha mfuko huo badala ya kuanzisha mifuko mipya sambamba na kuimarisha uwezeshaji wanawake kupitia miradi mbalimbali ya kisekta ya kukopesha wanawake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande mwingine, Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI iko katika hatua za mwisho za kuanza utoaji wa mikopo maalum kwa wanawake kupitia mradi wa pamoja utakaotekelezwa kwa ushirikiano na Benki ya Dunia, hatua itakayoongeza wigo kwa wanawake wengi kunufaika na mikopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuimarisha uwezeshaji wanawake kiuchumi kwa kushirikiana na sekta binafsi, taasisi za fedha na wadau wa maendeleo.