Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 23 | Community Development, Gender and Children | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 266 | 2026-05-06 |
Name
Tamima Haji Abass
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TAMIMA HAJI ABASS aliuliza: -
Je, Serikali ina mkakati gani wa kutoa elimu kuhusu uwepo wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) ili wanawake wengi zaidi wanufaike na mikopo?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tamima Haji Abass kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya mikakati ya Serikali ya kutoa elimu kuhusu uwepo wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF), ili wanawake wengi zaidi wanufaike na mikopo hiyo ni pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali, zikiwemo taasisi za fedha, kutoa mafunzo ya ujasiriamali na uendeshaji wa biashara kupitia makongamano ya kiuchumi ambayo hufanyika kikanda; kushirikiana na Wizara ya Fedha, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi; na kufanya mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Wizara inaendelea kuitaarifu mikoa na halmashauri juu ya uwepo wa mfuko huu na kuwaelekeza wafikishe taarifa husika kwa wananchi kupitia njia mbalimbali za mawasiliano, pamoja na kupitia majukwaa ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa na wananchi, ambapo watekelezaji wakuu wa kazi za mfuko huu ni Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi zote.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved