Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 42 Water and Irrigation Wizara ya Maji 504 2026-06-03

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question


MHE. KANGI A. LUGOLA K.n.y. MHE. ESTER A. BULAYA aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka fedha zilizobaki za utekelezaji wa miradi tisa ya maji yenye thamani ya shilingi bilioni 13 ambapo zimetolewa shilingi bilioni saba tu?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ester Amos Bulaya, Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa jumla ya miradi nane katika Jimbo la Bunda Mjini, Mkoani Mara kwa gharama ya jumla ya shilingi 21,671,846,983.12 ambapo hadi kufikia sasa jumla ya shilingi bilioni 13.7 zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo. Serikali itaendelea kutoa kipaumbele cha kupeleka fedha za utekelezaji wa miradi hiyo kwa hati ya madai zinazowasilishwa na kadri fedha zinavyopatikana ili iweze kukamilika kwa wakati na ubora stahiki. Ahsante sana.