Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kangi Alphaxard Lugola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Primary Question

MHE. KANGI A. LUGOLA K.n.y. MHE. ESTER A. BULAYA aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka fedha zilizobaki za utekelezaji wa miradi tisa ya maji yenye thamani ya shilingi bilioni 13 ambapo zimetolewa shilingi bilioni saba tu?

Supplementary Question 1

MHE. KANGI A. LUGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tunaishukuru Serikali ya Mheshimiwa Mama Samia kwa kutupatia shilingi bilioni saba Wananchi wa Bunda Mjini ili miradi hiyo iweze kukamilika. Pamoja na hayo Wananchi wa Bunda Mjini wanategemea mradi mmoja tu wa Nyabehu ambao ndiyo unawapatia maji, lakini kwa miezi ya hivi karibuni kumekuwa na upotevu wa maji kwa mabomba kupasuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali haioni haja ya kuchukua hatua za haraka kupeleka fedha ili kuweza kudhibiti upoteaji wa maji ili Wananchi wa Bunda Mjini wapate maji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Vijiji vya Sikiro, Mugara, Nyarugoma, Isanju, Mwiruruma na Muhula, Muranda, Chingurubira pamoja na Karukekere vinategemea Mradi wa Maji wa Isanju ambao kwa miezi minne sasa pampu ilikuwa imeharibika. Hata hivyo, taarifa tulizonazo ni kwamba pampu hii ilishakuja zaidi ya miezi miwili. Sasa kama hii pampu siyo pampu hewa ni sababu gani zinasababisha pampu hiyo isifungwe ili wananchi hawa waweze kupata maji? Ahsante sana.

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ester Amos Bulaya ambayo yameulizwa na Mbunge wa Mwibara, Mheshimiwa Kangi Lugola, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua umuhimu wa kukamilisha miradi ya maji nchini na kwa vile kukamilisha miradi ya maji nchini siyo mafanikio ya Serikali pekee bali ni ushindi kwa Watanzania wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunatambua umuhimu huo, lakini pia mradi huu ambao Mheshimiwa Mbunge ameuongelea kuhusu upotevu wa maji kwa sababu ya mabomba kupasuka, nimtoe hofu, mradi huu tayari tumeshaanza kuurekebisha, mabomba ya zamani yaliyokuwa yanafanya kazi pale yalikuwa GRP sasa tumeyabadilisha na sasa tunaweka steel pipes.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi nimepata picha ya kuonesha tayari kuna kilometa 2.1 tayari wameshayabadilisha hayo mabomba na tunaendelea na kilometa nyingine ambazo ni zaidi ya kama kilometa nne hivi. Kwa hiyo, tunaamini kwamba kwa kasi ambayo wanaenda nayo ndani ya muda mfupi bomba hilo litakuwa limerekebishwa na upotevu wa maji hautokuwepo tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo tunaendelea kuboresha taasisi zetu na usimamizi wa wataalamu wetu. Mheshimiwa Waziri wa Maji jana amefanya marekebisho na kufanya maboresho katika utendaji wa sekta yetu ya maji ikiwemo Bunda Mjini pamoja na maeneo mengine. Lengo ni kuhakikisha kuongeza tija katika utendaji wao na kuhakikisha kwamba wanachukua hatua za haraka tatizo linapotokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili la pampu ambalo Mheshimiwa Mbunge ameliongelea, sioni sababu pampu iwe imenunuliwa miezi miwili na ikawa bado haijafungwa na mtendaji wetu yuko pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi natoa maelekezo kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri, ninataka ndani ya wiki hii kama hakuna any technical problem zingine ambazo zinaambatana na uwepo wa ile pampu, basi pampu hiyo iwe imeshafungwa na vijiji vitano vya Mheshimiwa Mbunge waendelee kupata huduma ya maji safi na salama. Kinyume cha hapo tutachukua hatua kali zaidi kuhakikisha kwamba watendaji wanaendelea kujirekebisha na kuchukua hatua pale tatizo linapokuwa linajitokeza. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Stella Alex Ikupa

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KANGI A. LUGOLA K.n.y. MHE. ESTER A. BULAYA aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka fedha zilizobaki za utekelezaji wa miradi tisa ya maji yenye thamani ya shilingi bilioni 13 ambapo zimetolewa shilingi bilioni saba tu?

Supplementary Question 2

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kutokana na changamoto ya kupasuka kwa mabomba, changamoto ambayo inasababisha upotevu wa maji, Serikali inaonaje ikaanzisha namba maalumu ya kuripoti changamoto hiyo? Kwa sababu mara nyingi mimi nimekuta maji yanamwagika na ukiuliza wahusika wanasema hawajui mahali pa kuripoti. La kwangu ni hilo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Stella Ikupa unaweza ukarudia swali lako na Waheshimiwa Wabunge tunaomba tupunguze sauti ili muuliza swali na mjibu swali waweze kusikilizana.

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na changamoto ya kupasuka kwa mabomba, changamoto ambayo inapelekea upotevu wa maji, Serikali inaonaje ikaanzisha namba maalumu kwa ajili ya kuripoti changamoto hiyo inapotokea? Kwa sababu kuna maeneo ukipita ukakuta maji yanamwagika kutokana na kwamba bomba limepasuka ukiuliza wahusika wanasema kwamba hawajui wanaripoti wapi. Ahsante.

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Stella, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni swali muhimu sana na linajenga msingi imara wa ushirikishwaji wa wananchi pale wanapoona kuna miundombinu imepata changamoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa tayari tuna hizo namba isipokuwa naona kwamba tutabadilisha namna ya kuhakikisha kwamba namba hizi zinafahamika kwa wananchi. Lengo ni kwamba tuweze kushirikiana kutoa taarifa pale ambapo mabomba yanakuwa yamepasuka na kuweza kuokoa maji yanayopotea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napokea ushauri wa Mheshimiwa Stella na kwa umuhimu wake, ahsante sana.

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. KANGI A. LUGOLA K.n.y. MHE. ESTER A. BULAYA aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka fedha zilizobaki za utekelezaji wa miradi tisa ya maji yenye thamani ya shilingi bilioni 13 ambapo zimetolewa shilingi bilioni saba tu?

Supplementary Question 3

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Katika Jimbo la Bunda kuna Mradi wa Nyamuswa una shilingi bilioni nane, umekwama hauendelei; Mradi wa Hunyari shilingi milioni 830, umekwama hauendelei; na Mradi wa Lambo la Mihingo shilingi bilioni 1.5 umekwama hauendelei. Ni lini sasa Waziri tutakaa na wewe na wakuu wa RUWASA wa mkoa na wilaya tujadili miradi ya Jimbo la Bunda?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Getere, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Getere ameomba ni lini tutakaa na viongozi wa wilaya na mkoa. Sisi tuko tayari dakika yoyote na Wizara itakupatia ushirikiano pale ambapo tutakaa na kupanga tarehe maalumu na kufanya mwaliko ili wahusika ambao umewataja tuweze kukaa nao kwa pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, tunatambua kuna utekelezaji wa miradi ndani ya Jimbo la Bunda, lakini sambamba na hilo tunafahamu kwamba kuna uhitaji wa fedha ikiwemo Mradi wa Nyamuswa ambapo na mimi niliweza kufika katika mradi huo naufahamu vizuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, juzi hapa Wizara ya Maji tumepeleka kiasi cha shilingi milioni 200 kwa ajili ya miradi hiyo hiyo ambayo inaendelea kutekelezwa ndani ya Jimbo la Bunda. Nikutoe hofu, sambamba na kikao ambacho umekiomba Serikali bado itaendelea kufanya juhudi za haraka sana kuendelea kuhakikisha kwamba tunawafikishia huduma ya maji safi na salama kwa kupeleka fedha katika miradi inayoendelea ili iweze kukamilika. Ahsante sana.