Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 42 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 505 | 2026-06-03 |
Name
Yustina Arcadius Rahhi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. YUSTINA A. RAHHI aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Mradi wa Maji wa Tsoray utakaohudumia vijiji 21 katika Halmashuri ya Mji wa Mbulu?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Yustina Arcadius Rahhi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kutafuta fedha zaidi ya shilingi bilioni 70 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Kimkakati wa Tsoray uliopo Tarafa ya Nambis, Wilaya ya Mbulu, Mkoani Manyara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni mwa kazi zinazotarajiwa kutekelezwa kupitia mradi huo ni pamoja na ujenzi wa chanzo cha maji chenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 13.6 kwa siku, ujenzi wa nyumba ya mitambo (pump house), ununuzi na ufungaji wa pampu nne za kusukuma maji, ujenzi wa matanki nane yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 6.6, ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 429.5, ujenzi wa vituo 160 vya kuchotea maji sambamba na ujenzi wa mbauti (cattle trough) sita za kunyweshea mifugo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huo ukianza kutekelezwa unatarajiwa kuchukuwa miezi 24 ambapo unalenga kunufaisha zaidi ya wananchi 109,228 waishio kwenye vijiji 21 vya Wilaya ya Mbulu. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved