Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 42 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 506 2026-06-03

Name

Florent Laurent Kyombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE. FROLENT L. KYOMBO aliuliza: -

Je, lini Serikali itatenga bajeti ya kutosha ili kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Katoma – Bukwali badala ya kujenga mita 200 kila mwaka?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Florent Laurent Kyombo, Mbunge wa Missenyi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea na ujenzi wa Barabara ya Katoma – Bukwali kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Hadi sasa jumla ya kilometa 8.2 kati ya kilometa 39.83 zimejengwa kwa kiwango cha lami. Kwa sehemu iliyobaki kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina inaendelea na imefikia 65%. Baada ya usanifu kukamilika, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi. Ahsante.