Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 42 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 507 | 2026-06-03 |
Name
Silvery Luboja Salvatory
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Primary Question
MHE. SILVERY L. SALVATORY aliuliza:
Je, lini upanuzi wa barabara kuu kwa njia nne kutoka Kenyatta – Usagara Mwanza utaanza?
Name
Abdallah Hamis Ulega
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkuranga
Answer
WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Silvery Luboja Salvatory, Mbunge wa Misungwi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya upanuzi wa Barabara ya Mwanza Mjini hadi Usagara imekamilika ambapo itahusisha urefu wa kilometa 25 kutoka njia mbili zilizopo sasa kwenda njia nne. Kwa sasa utaratibu wa manunuzi wa kumpata mkandarasi wa ujenzi wa barabara unaendelea. Kazi ya ujenzi itaanza mara moja baada ya mkandarasi kuwa amepatikana, naomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved