Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 16 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 186 2026-04-24

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kufuatilia maendeleo ya Wanafunzi wanaofanya vizuri kitaifa ili kuhakikisha wanakuwa rasilimali muhimu kwa maendeleo ya Taifa?

Name

Prof. Adolf Faustine Mkenda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rombo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) K.n.y. WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inathamini na kufuatilia maendeleo ya wanafunzi wanaofaulu vizuri katika mitihani ya Kitaifa kwa kuwa, ni rasilimali muhimu kwa maendeleo ya nchi. Katika kutekeleza jitihada hizo, Serikali imeweka mpango mahsusi wa kubaini na kufuatilia maendeleo yao, sambamba na kuwaendeleza kitaaluma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, kupitia Mpango wa Samia Scholarship Serikali katika mwaka wa fedha 2025/2026 imetoa ufadhili kwa wanafunzi 936 waliofaulu vizuri katika mitihani ya Kidato cha Sita, hususan katika masomo ya Sayansi na Hisabati. Lengo ni kuwaendeleza katika maeneo ya kimkakati katika sayansi, teknolojia, uhandisi na tiba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia ufadhili wa Samia Scholorship Extended jumla ya wanafunzi 50 wamepelekwa katika Chuo Kikuu cha Johannesburg, Afrika Kusini na Chuo Kikuu cha Limerick, nchini Ireland, kwa ajili ya kusomea masomo ya Sayansi ya Kompyuta, Hisabati ya Juu na Akili Unde (Artificial Intelligence). Serikali itaendelea kuongeza wigo wa kufuatilia na kuwaendeleza wanafunzi wanaofanya vizuri katika mitihani ya Kitaifa ili waweze kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya Taifa, ahsante.