Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 16 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 188 2026-04-24

Name

Hamoud Abuu Jumaa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibaha Vijijini

Primary Question

MHE. HAMOUD A. JUMAA aliuliza: -

Je, lini Serikali italipa fedha za kuanza kazi kwa Mkandarasi wa ujenzi wa Barabara ya Mlandizi hadi Ruvu SGR Station, ili ujenzi uanze rasmi?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Hamoud Abuu Jumaa, Mbunge wa Kibaha Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Mlandizi hadi Stesheni ya Ruvu SGR, yenye urefu wa kilomita 23, inaunganisha Barabara Kuu ya Morogoro, yaani TANZAM, katika eneo la Mlandizi na Stesheni ya SGR ya Ruvu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, Serikali imeingia mkataba na mkandarasi wa ujenzi wa barabara hiyo kwa utaratibu wa sanifu na jenga, yaani design and build, ambapo ujenzi wa barabara hiyo unatarajia kukamilika mwezi Januari, 2028. Kwa sasa, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kumlipa mkandarasi malipo ya awali, ili aweze kuanza kazi, ahsante.