Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Hamoud Abuu Jumaa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibaha Vijijini
Primary Question
MHE. HAMOUD A. JUMAA aliuliza: - Je, lini Serikali italipa fedha za kuanza kazi kwa Mkandarasi wa ujenzi wa Barabara ya Mlandizi hadi Ruvu SGR Station, ili ujenzi uanze rasmi?
Supplementary Question 1
MHE. HAMOUD A. JUMAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri, lakini kuna swali moja dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, bado Serikali haijapata fedha, na kawaida wakati unakuwa na mambo makubwa; unakuwa na mpango wa muda mrefu na mpango wa muda mfupi. Sasa, barabara yetu hii kwa sasa haipitiki na ni barabara ambayo tunaitegemea kiuchumi. Je, Serikali ina mpango gani kwa sasa kuitengeneza hii barabara, ili iweze kupitika kwa muda wote?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba, barabara nyingi hasa ambazo zimejengwa kwa kiwango cha changarawe zimekuwa na changamoto katika kipindi cha mvua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamkumbusha Mheshimiwa Mbunge pia kwamba, barabara hii ilikuwa na vipande viwili. Kilomita hizi nyingine nane zilikuwa zinahudumiwa na wenzetu wa TARURA ambapo sasa zimeunganishwa kwa pamoja, na kuwa zinakwenda kujengwa na TANROADS.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa, ninatoa maelekezo kwa Meneja wa Mkoa wa Pwani kwamba, kwa kuwa stesheni ya Ruvu SGR wananchi wengi wanaitumia hasa wa Mkoa wa Pwani maeneo ya Kibaha na Mlandizi, ahakikishe barabara hii inapitika muda wote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ikiwezekana leo ama kesho aweze kuitembelea hiyo barabara, ili maeneo yote ambayo yanaifanya isipitike aweze kuyasimamia na kuweka mkandarasi kwa haraka, ili wananchi ambao wanatumia hicho kituo cha Ruvu SGR waweze kupata hiyo huduma. Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Songea Mjini
Primary Question
MHE. HAMOUD A. JUMAA aliuliza: - Je, lini Serikali italipa fedha za kuanza kazi kwa Mkandarasi wa ujenzi wa Barabara ya Mlandizi hadi Ruvu SGR Station, ili ujenzi uanze rasmi?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. DAMAS D. NDUMBARO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Barabara ya mchepuko, kilomita 16, ndani ya Jimbo la Songea Mjini wananchi bado hawajalipwa fidia. Je, ni lini Serikali italipa fidia, ili ujenzi wa barabara hiyo uweze kuanza? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tuna barabara ya kilomita 16 ambayo sisi tunasema ni Songea Bypass. Barabara hii inajengwa na Serikali ya Tanzania kwa kusaidiana na World Bank. Tayari tumeshafanya uthamini wa wananchi ambao watapisha mradi huo ambao ni zaidi kidogo ya shilingi bilioni Nne.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamhakikishia Mheshimiwa Ndumbaro pamoja na wananchi wa Songea kwamba tunategemea Serikali kulipa fidia hiyo ambayo tayari ipo Hazina ili mradi huo uanze.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa hiyo barabara ya bypass pia mkandarasi huyo ndiye atakayejenga kutoka Songea kilometa 100 kuelekea Njombe hadi Lutukira tayari ameshaanza kazi, yuko kwenye hatua za awali kwa maana ya mobilization, atakapokuwa anaendelea, basi tukishalipa ataanza pia kujenga hicho kipande cha bypass ili magari mengi yanayopita hapo na hasa ya makaa ya mawe kwenda huko Mtwara yasiweze kupita Songea Mjini, ahsante.
Name
Zuena Athumani Bushiri
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAMOUD A. JUMAA aliuliza: - Je, lini Serikali italipa fedha za kuanza kazi kwa Mkandarasi wa ujenzi wa Barabara ya Mlandizi hadi Ruvu SGR Station, ili ujenzi uanze rasmi?
Supplementary Question 3
MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Lembeni – Nyumba ya Mungu inayokwenda katika mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe haijawekwa lami. Je, ni upi mpango wa Serikali wa kuweka lami katika barabara hiyo?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Serikali inatafuta fedha ya kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami, tunachofanya ni kuhakikisha kwamba hiyo barabara inapitika. Kwa hiyo, ninamwagiza Meneja wa TANROADS kuhakikisha kwamba barabara hiyo aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge inapitika katika kipindi hiki hasa kwa dharura, lakini baada ya mvua kwisha, basi barabara hii iweze kujengwa katika hali ambayo inaweza ikapitika kwa muda wote. Ahsante.
Name
Paschal Inyasi Chinyele
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Dodoma mjini
Primary Question
MHE. HAMOUD A. JUMAA aliuliza: - Je, lini Serikali italipa fedha za kuanza kazi kwa Mkandarasi wa ujenzi wa Barabara ya Mlandizi hadi Ruvu SGR Station, ili ujenzi uanze rasmi?
Supplementary Question 4
MHE. PASCHAL I. CHINYELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona. Serikali ipo katika hatua za mwisho za kufanya upanuzi wa barabara tatu zinazokwenda Mikoa ya Iringa - Singida pamoja na Arusha. Hata hivyo, Serikali bado hawajalipa fidia wakazi wa Jiji la Dodoma hasa katika Kata za Kikuyu, Mkonze, Mnadani, Nala, Chamwino, Mnadani pamoja na Miyuji. Je, Serikali ina mpango gani kuwalipa wakazi hao kabda ya upanuzi wa barabara hizi haujaanza?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninamshukuru Mheshimiwa Chinyele kwa kufuatilia ulipaji wa fidia wa wananchi wake kwa wale hasa ambao watapitiwa na miradi ya kupanua barabara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Serikali ipo kwenye hatua za mwisho kuanza kujenga barabara ya njia nne kutoka katikati ya Jiji kwenda njia ya Dar es Salaam, kwenda njia ya Arusha, na pia kwenda njia ya Iringa ili kupunguza msongamano.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, tumeshaanza kufanya uthamini kwa maana ya wananchi watakaopisha mradi, na tutahakikisha kwamba hatumbomolei mwanachi yeyote ambaye amefuatwa na barabara kabla hatujamlipa fidia. Kama kuna changamoto mahali popote kwenye Kata yoyote, Mheshimiwa Mbunge tunaomba tuwasiliane ili tuweze kufika na kuondoa changamoto kwa sababu ni utaratibu mwananchi yeyote anapopisha ujenzi wa barabara, anastahili kulipwa fidia, ahsante.
Name
Asha Ramadhani Baraka
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAMOUD A. JUMAA aliuliza: - Je, lini Serikali italipa fedha za kuanza kazi kwa Mkandarasi wa ujenzi wa Barabara ya Mlandizi hadi Ruvu SGR Station, ili ujenzi uanze rasmi?
Supplementary Question 5
MHE. ASHA R. BARAKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Barabara Kibaha DC yenye kilometa 34 ni barabara ambayo haipitiki, siyo rafiki na ina vitu muhimu sana. Kuna Kituo cha Afya cha Halmashauri na kuna shule ya Primary yenye watoto wenye mahitaji maalum na pia kuna uwanja mkubwa sana ambao mikutano yote inafanyika hapo ya Kibaha DC, na shughuli zote ikiwemo na burudani. Je, Serikali ina mpango gani wa kuijenga hiyo barabara kwa kiwango cha lami? Ni lini?
MWENYEKITI: Majibu, Mheshimiwa Naibu Waziri.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, maswali yake nimeyaelewa, lakini barabara aliyoitaja ndiyo sijaisikia vizuri.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Asha Baraka, taja tu barabara.
MHE. ASHA R. BARAKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara inaitwa kwa jina maarufu Makofia – Mlandizi yenye kilometa 34 ambayo inaunganisha hospitali kubwa dispensary kubwa ambayo wanatumia watu wa Mlandizi.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Makofia – Mlandizi nadhani itakuwa ni swali la tatu ama la nne katika session hii ya Bunge kuulizwa. Barabara hii tumeijibu na tutaendelea kujibu kwamba ni barabara ambayo ni muhimu sana kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tulikuwa tumefanya tathmini ya fidia awali, lakini ikaonekana muda umepita. Tumefanya tena uthamini upya ambao jedwali la malipo ya fidia iko Hazina kwa ajili ya kuwalipa hao wananchi ambao watapisha barabara ili hii barabara iweze kujengwa, ahsante.
Name
Jackson Gedion Kiswaga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalenga
Primary Question
MHE. HAMOUD A. JUMAA aliuliza: - Je, lini Serikali italipa fedha za kuanza kazi kwa Mkandarasi wa ujenzi wa Barabara ya Mlandizi hadi Ruvu SGR Station, ili ujenzi uanze rasmi?
Supplementary Question 6
MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Je, ni lini Serikali itaunganisha kwa lami kati ya Kijiji cha Ihemi na Kijiji cha Mgama ambapo kuna kilometa kama sita hivi zilizobaki? Ahsante sana.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali hili pia liliulizwa na Mbunge wa Kilolo ambayo nadhani hiyo barabara ikitoka Ihemi – Mgama inaenda pia na Kilolo. Ni barabara ambayo inahudumiwa na wakala wetu na iko kwa kiwango cha changarawe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati tunatafuta fedha ya kuijenga hiyo barabara kwa kiwango cha lami, tunachoweza kumwahidi Mheshimiwa Mbunge ni kwamba tutahakikisha kwanza inapitika kwa kipindi chote cha mwaka wakati Serikali inatafuta fedha ili kuweza kukamilisha usanifu na kuijenga kwa kiwango cha lami, ahsante.