Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 16 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 189 2026-04-24

Name

Masache Njelu Kasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupa

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: -

Je, lini ujenzi wa barabara kutoka Makongolosi hadi Rungwa kwa kiwango cha lami utaanza?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Masache Njelu Kasaka, Mbunge wa Lupa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Makongolosi – Rungwa (km 176.51) ni sehemu ya barabara ya Mbeya – Rungwa (Km 288.9). Ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi sasa ujenzi wa sehemu ya Mbeya - Makongolosi (km 112.39) kwa kiwango cha lami umekamilika. Kwa sehemu iliyobaki, yaani Makongolosi – Rungwa (km 176.51) Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi. Ahsante.