Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Latifa Khamis Juwakali

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. LATIFA KHAMIS JUWAKALI aliuliza:- Je, kipi kipaumbele cha Wizara ya Vijana kwa vijana wa Tanzania?

Supplementary Question 1

MHE. LATIFA KHAMIS JUWAKALI: Mheshimiwa Spika, ninamshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri ambayo yanalenga kuwatia moyo vijana, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; Mheshimiwa Waziri ni kiasi gani cha fedha kimetengwa kupitia Mfuko huu wa Maendeleo wa Vijana Taifa katika mwaka huu wa fedha?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; ili kuwasaidia na kuweka ahueni kwa vijana, Wizara haioni haja sasa ya kuya-hold hayo mashirika na maeneo mbalimbali ambayo wanataka kuwasaidia vijana ili waanzishe SACCOS maalum kwa vijana wa nchi hii na kupunguza zile afueni kwa ajili ya vijana ikiwemo riba? Ahsante.

Name

Joel Arthur Nanauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtwara Mjini

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MAENDELEO YA VIJANA: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Latifa, Mbunge wa Viti Maalum kwamba Serikali kwa miaka yote kupitia Idara ya Vijana iliyokuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa ikitenga bajeti kwa ajili ya uwezeshaji wa vijana, lakini utakumbuka kwamba Mheshimiwa Rais alielezea dhamira yake ya kuona namna anavyoongeza mitaji kwa ajili ya vijana katika kuwawezesha kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, ninapenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba dhamira hiyo ipo na Serikali muda mfupi ujao itatoa mpangilio wa namna ambavyo vijana wa Tanzania watanufaika na mitaji ambayo itatolewa na Serikali.

Mheshimiwa Spika, pili Wizara yetu itaendelea kuratibu, kushirikiana na mashirika na wadau mbalimbali ambao wanajishughulisha na shughuli za vijana, nia na dhamira ikiwa ni kukusanya nguvu za pamoja kuwawezesha vijana katika nchi yetu sawasawa na Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 ambayo uliboreshwa mwaka 2024. Ahsante sana.

Name

Janeth Elias Mahawanga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. LATIFA KHAMIS JUWAKALI aliuliza:- Je, kipi kipaumbele cha Wizara ya Vijana kwa vijana wa Tanzania?

Supplementary Question 2

MHE. JANETH E. MAHAWANGA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa nafasi. Je, ni kwa namna gani Serikali imejipanga kuhakikisha vijana wa mijini na vijijini wanashiriki kikamilifu katika Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050? (Makofi)

Name

Joel Arthur Nanauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtwara Mjini

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MAENDELEO YA VIJANA: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Janeth Mahawanga. Serikali kupitia Sera ya Maendeleo ya Vijana imeweka mkakati maalum wa utekelezaji wa ushiriki wa vijana wa mijini na vijijini pia rika zote na wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutekeleza afua hizo na kuhakikisha kila kijana wa Tanzania anakuwa sehemu ya mambo muhimu yanayofanywa katika Taifa letu. Ahsante.