Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Charles Mhando Njama
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Korogwe Mjini
Primary Question
MHE. CHARLES M. NJAMA aliuliza:- Je, lini barabara ya Old Korogwe – Kwamndolwa kilomita 10 itajengwa kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 1
MHE. CHARLES M. NJAMA: Mheshimiwa Naibu Spika, Ninashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina swali moja la nyongeza. Je, kilomita 2.45 za kutoka Korogwe Girls – Stesheni zitafanyiwa upanuzi ili kuendana na ujenzi wa barabara mpya kutoka Old Korogwe – Kwamndolwa? Ahsante.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimjibu Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, tunapoanza hii barabara ni kuanzia Old Korogwe – Kwamndolwa. Nimwelekeze Meneja wa Mkoa wa Tanga kwamba kwa kuwa hii barabara inaenda Korogwe Girls waende wakaiangalie na kuona kama imefanyiwa usanifu ama kama haijafanyiwa usanifu iweze kufanyiwa usanifu ili tuweze kuunga hizo kilometa 2.5 kwa kiwango cha lami. Ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved