Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

John Francisco Nzilanyingi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyamagana

Primary Question

MHE. JOHN F. NZILANYINGI aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Uwanja wa Ndege Mwanza utakamilika ili uwe na hadhi ya Kimataifa?

Supplementary Question 1

MHE. JOHN F. NZILANYINGI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana kwa majibu ya Serikali, lakini ninaomba sasa niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; ninaomba kufahamu, huo upembuzi yakinifu unahusisha kitu gani na utakamilika lini? Kwa sababu tarehe 28 Machi, 2024, Serikali ilisaini mkataba na mkandarasi anayeitwa Taifa Civil Mining Limited, mkataba ambao ulikuwa na zaidi ya thamani ya bilioni 29.

Mheshimiwa Spika, kwa maelezo ya Serikali, wananchi wa Nyamagana, nikiwemo mimi mwenyewe kama mwakilishi wao, ninapata mkanganyiko wa nini ambacho kinaendelea kufanyiwa upembuzi yakinifu, ilhali Serikali tayari imekwishasaini mkataba.

Mheshimiwa Spika, swali la pili; toka Serikali isaini mkataba huo, haijawahi kupeleka hata senti tano. Hivi ninavyozungumza, kwa taarifa nilizonazo, mkandarasi ameanza kuondoa vifaa vyake site. Ni lini sasa Serikali itapeleka fedha ili mkandarasi aweze kuendelea na kazi ya ujenzi wa uwanja? Ahsante. (Makofi)

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, kwanza ninampongeza sana Mheshimiwa Nzilanyingi kwa ufuatiliaji wake wa karibu kwenye uwanja wetu huo wa Mwanza, lakini yeye Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wote wa Mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla, wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wananchi kwa ujumla. Kiko kilio kimoja ambacho wamekuwa wakikitoa kwa muda mrefu, ni lini uwanja wa Mwanza utapewa hadhi ya kimataifa.

Mheshimiwa Spika, kufuatia maombi hayo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Samia Suluhu Hassan, amepokea kilio hicho na amefanya usanifu, ametuelekeza kama sekta chini ya Waziri wetu Mheshimiwa Mbarawa tumefanya tathmini ya kina na kubaini kuwa, iko haja kubwa ya kuufanya uwanja kuwa wa kimataifa.

Mheshimiwa Spika, sasa mambo mazuri yanahitaji pia subira, nini kinafanyika kama nilivyosema? Mambo matatu; la kwanza Jengo lilopo kwa sasa, linatosha abiria karibu 400,000 – 500,000. Tunataka tufanye usanifu ili tuweze kujenga jengo kubwa litakaloweza kubeba abiria zaidi ya milioni mbili na laki tano. Ili ndani ya jengo, tuweze kuweka taasisi zote muhimu ambazo ni sifa na takwa muhimu kwenye uwanja wa kimataifa; Uhamiaji, Afya, pamoja na Maliasili na vitu vingine vingine. Mbili, runway; ili uwanja uweze kuwa wa kimataifa, ule upana wake hautoshi. Tunaongeza kutoka meta 45 mpaka meta 60 na ku-maintain urefu uliopo wa takribani meta 3,800.

Mheshimiwa Spika, la tatu, ni taa. Ule uwanja uliopo awali tulifikiri pengine zile taa zingetosha, lakini baada ya tathmini ya kina, inaonekana kabisa kwamba zile taa hazitatosha kwa sababu zilijengwa miaka ya 1970. Hivyo basi, tunataka tubadilishe taa zilizopo na kuweka za kisasa. Kwa sababu hiyo nimwombe Mheshimiwa Mbunge pamoja na Wabunge wote waweze kuwa na subira.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, ameuliza kwamba Serikali haikupeleka fedha ni kweli na jengo lililopo linafanya nini? Jengo lililopo sasa ambalo tulikuwa tumeshaanza ujenzi ambao tunashirikisha sekta binafsi tutalitumia kwa ajili ya general aviation. ndege ndogo, wale watu wa premium, ukiwa na ndege yako, utatumia jengo hilo. Lengo ni jema tu, kuhakikisha kwamba tunaupa hadhi ya kimataifa na inayostahili uwanja huo ambao unasafirisha bidhaa mbalimbali kutoka nchini kwetu minofu ya samaki, maliasili pamoja na utalii, kwa maana ya utalii kwa ujumla na kadhalika. (Makofi)

Name

John Francisco Nzilanyingi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyamagana

Primary Question

MHE. JOHN F. NZILANYINGI aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Uwanja wa Ndege Mwanza utakamilika ili uwe na hadhi ya Kimataifa?

Supplementary Question 2

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana kwa nafasi. Hitaji la Uwanja wa Ndege wa Njombe ni kubwa sana kutokana na uchumi wa Njombe, lakini ni mradi wa kimkakati, pia ni ahadi Rais, ni lini sasa ujenzi wa uwanja huu utaanza?

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mheshimiwa Mwanyika kwa ufuatiliaji wake wa karibu sana juu ya Uwanja wa Ndege wa Njombe. Yeye na Wabunge wenzake wa Mkoa wa Njombe wanafanya kazi nzuri. Serikali imetambua na kuthamini umuhimu wa uwanja wa Njombe kama nilivyosema kwenye kubebea mazao kama vile parachichi na kadhalika na kwa sababu hiyo, Serikali inakwenda kujenga uwanja mkubwa. Ni hatua gani tuko mpaka sasa hivi?

Mheshimiwa Spika, tayari tulikuwa kwenye hatua ya kwanza ya kutafuta eneo, kwa sababu eneo la pale mjini halitoshi. Tayari viongozi wa mkoa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege wanashirikiana. Hatua ya pili tunayokwenda sasa ni kwa ajili ya kufanya usanifu ili tuweze kujua kiasi gani kinachohitajika uwanja utakaojengwa uweze kwenda sawasawa na hadhi ya Mkoa wa Njombe.

Name

William Kafiti Kafiti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Primary Question

MHE. JOHN F. NZILANYINGI aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Uwanja wa Ndege Mwanza utakamilika ili uwe na hadhi ya Kimataifa?

Supplementary Question 3

MHE. KAFITI W. KAFITI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa nafasi hii ya kuuliza swali la nyongeza. Kutokana na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, bado sisi kama Mwanza na kama wakazi wa Jimbo la Ilemela, tunahitaji kujua huo upembuzi yakinifu utakamilika lini?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, ukamilishwaji wa uwanja huu...

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kafiti Mbunge wa Ilemela alikuwa anajaribu kukazia hoja ile ile ya uwanja wa ndege na kimsingi yeye pale kwake hoja kubwa ambayo anaizungumzia ni upande wa fidia au namna ya kuweza kuondoa wananchi wa pale. Serikali ina dhamira ya kuufanya Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuwa wa kimataifa. Ili uweze kuwa na sifa hizo, lazima kama kuna wavamizi waondolewe. Kwa hiyo, nimwombe tu awe na subira, tutamilisha muda siyo mrefu tutaanza kufanya kazi.

Name

Bonnah Ladislaus Kamoli

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Segerea

Primary Question

MHE. JOHN F. NZILANYINGI aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Uwanja wa Ndege Mwanza utakamilika ili uwe na hadhi ya Kimataifa?

Supplementary Question 4

MHE. BONNAH L. KAMOLI: Mheshimiwa Spika, pamoja na kazi nzuri ambayo inafanywa, Mkoa wa Dar es Salaam especially Kipunguni ambako Serikali imefanya kazi kubwa kuwalipa wananchi wa pale, lakini bado kuna wananchi ambao wanahitaji kulipwa ili waondoke. Je, ni lini Serikali itawamalizia hawa wananchi wa Kipunguni pesa zao ili waweze kuondoka maana hapo kuna mateso makubwa? Ninashukuru.

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kujibu tena swali lingine la Mheshimiwa Bonnah, Mbunge wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kazi ambayo alishaianza huko mwanzoni kwa ajili ya wananchi wa Kipunguni. Kama tunavyofahamu wananchi hawa wamekuwa wakidai fidia zao kwa miaka mingi sana, lakini ni Dkt. Samia Suluhu Hassan, mara baada ya kuingia na mpaka mwaka jana kati ya fedha walizokuwa wanazidai amekwishalipa bilioni 66 kwa wananchi karibu 717 kati ya 1,147. Nimwombe Mheshimiwa Bonnah na Wabunge wote wa Mkoa wa Dar es Salaam wavumilie, wale waliobakia watakwenda kulipwa kadri ya upatikanaji wa fedha Serikalini.

Name

Masanja Kungu Kadogosa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Vijijini

Primary Question

MHE. JOHN F. NZILANYINGI aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Uwanja wa Ndege Mwanza utakamilika ili uwe na hadhi ya Kimataifa?

Supplementary Question 5

MHE. MASANJA K. KADOGOSA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa hii fursa. Serikali ilifanya tathmini ya uwanja wetu wa Simiyu eneo la lgegu na hiyo tathmini ilifanyika kwa takribani miaka minne iliyopita. Je, ni lini sasa Serikali itatoa fidia lakini vilevile kuanza ujenzi wa uwanja ule?

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mshimwa Spika, ninampongeza Mshimiwa Kadogosa kwa kufuatilia Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Simiyu kwa sababu pia ni sera za Serikali kuhakikisha kwamba angalau kila mkoa unaweza kupata uwanja wa ndege.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Serikali imeshakamilisha usanifu wa uwanja huo na tumebaini kwamba tunahitaji eka karibu 3,386 na wananchi 700 kama na 92 ambao tumewatambua pale kiasi wanachodai ni shilingi bilioni 6.2. Nimwombe avumilie. Mara baada ya upatikanaji wa fedha tutaweza kwenda kulipa eneo hilo. (Makofi)

Name

Esther Lukago Midimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOHN F. NZILANYINGI aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Uwanja wa Ndege Mwanza utakamilika ili uwe na hadhi ya Kimataifa?

Supplementary Question 6

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Mheshimiwa Kadogosa ameuliza ila ninataka kukazia hapo. Ni muda mrefu tunauliza kuhusu ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Simiyu na Uwanja ule ukikamilika watalii watakua wanashuka. Pale ni karibu kwenda Serengeti na Ngorongoro. Ni lini sasa uwanja huo utakamilika? Tunataka kauli ya Serikali kwa sababu ni muda mrefu eneo limeshatengwa. (Makofi)

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa swali la nyongeza la Mheshimiwa Midimu ambaye anasisitiza umuhimu wa Uwanja wa Ndege wa Simiyu. Kama nilivyokwishakujibu pale mwanzoni kwamba tayari tumekwishaainisha kiasi cha fidia kinachohitajika shilingi bilioni sita pamoja na wananchi ambao tunatakiwa tuwafidie na eneo lenyewe.

Mheshimiwa Spika, niwaombe Waheshimiwa Wabunge, mpango wa Serikali ni mzuri. Ukiangalia miaka mitano nyuma na sasa ni tofauti. Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imekwenda kujenga viwanja karibu vyote nchini. Ni maeneo machache sana ambayo hatujayafikia. Ukiangalia Kanda ya Ziwa peke yake ambapo Waheshimiwa wako huko: Shinyanga, Musoma, Serengeti (tunakwenda kuanza kujenga), Kyabajwa na Mwanza yenyewe. Ninaomba Ndugu zangu wavumilie, tunakwenda kufikia eneo hilo. (Makofi)

Name

Joseph Kasheku Musukuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita

Primary Question

MHE. JOHN F. NZILANYINGI aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Uwanja wa Ndege Mwanza utakamilika ili uwe na hadhi ya Kimataifa?

Supplementary Question 7

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika, ningependa kumwuliza swali la nyongeza Mheshimiwa Waziri. Mheshimiwa Naibu Waziri amesema lile jengo la Mwanza litabaki kama jengo la general aviation na lina mkataba wake na yeye amefanya upembuzi yakinifu kwa ajili kujenga jengo la international. Kama halivunjwi kwa nini mkandarasi anaondoka asimalizie lile jengo? Ninakushukuru. (Makofi)

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, tunaendelea na mazungumzo katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza ikiwezekana kujenga kwa kupitia mwekezaji binafsi (Sekta ya PPP) tushirikiane na mjenzi. Kwa hiyo, nimwombe awe na subira tukikamilisha taratibu atapata taarifa nzuri zaidi.