Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

John Francisco Nzilanyingi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyamagana

Primary Question

MHE. JOHN F. NZILANYINGI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara ya njia nne kutoka Mjini – Usagara na kutoka Mjini – Kisesa?

Supplementary Question 1

MHE. JOHN F. NZILANYINGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jiji la Mwanza ni jiji ambalo linakuwa kwa kasi sana na ukuaji wa jiji hili linaenda sambamba na ongezeko la watu jambo ambalo linapelekea kuwa na foleni kubwa sana. Naomba kufahamu kutoka Serikalini, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ni lini sasa tender ya ujenzi wa barabara ya kutoka Mwanza kwenda Usagara itatangazwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Jiji letu la Mwanza lina malango makuu mawili kwa maana ya njia ya Usagara Mjini pamoja na ya Mwanza - Kisesa. Ujenzi wa barabara hizi unapaswa kwenda sambamba kwa sababu ni barabara ambazo ni mapacha na yanategemeana sana kwa ukuaji wa uchumi wa jiji letu. Naomba kufahamu, tunavyoendelea na mchakato wa upande wa Mwanza – Usagara, ni lini sasa Mwanza - Kisesa nayo itawekwa kwenye mchakato wa kutangazwa ili iweze kujengwa kwa kiwango cha njia nne? Ahsante.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jibu la msingi nimesema tuko kwenye hatua za mwisho na kama tuko hatua za mwisho ni kwamba, tulishatangaza tender na mkandarasi alishapatikana. Tunachofanya sasa hivi ni majadiliano ama negotiations, kulingana na ukweli kwamba sisi tunakuwa na engineer estimate, yaani makadirio. Sisi tunategemea hiyo barabara itakwenda, itajengwa kwa kiasi gani na mkandarasi anakuja na bei zake ambazo tuko kwenye majadiliano ili tukikubaliana na sisi tutakuwa tuko tayari kumpa hiyo kazi ya kuanza ujenzi.

Kwa hiyo, hatua ya kutangaza tulishakamilisha, tuko kwenye majadiliano na mkandarasi ambaye tunadhani anaweza akatujengea hiyo barabara na tukishakamilisha, maana yake tutakuwa tunaanza ujenzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala lako la pili kwamba ziende sambamba na nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge, Jiji la Mwanza linakuwa sana, lakini kama nilivyosema kwamba, inategemea na uwezo wa kibajeti kwa wakati huo.

Kwa hiyo, kwa sasa tumeamua kwamba, kwanza tuanze na hiyo na kama fedha Serikali itapatikana na ndiyo maana tumeshasanifu na hata wakati tunafanya marekebisho ya pale Mabatini, tumejenga katika mtazamo huo huo wa njia nne, ambazo tunaamini barabara itakapoanza kujengwa, basi itafuata utaratibu huo huo. Kwa hiyo, ni matumaini yetu kwamba, tutaijenga pia hiyo Barabara ya Mwanza-Kisesa kwa njia nne. Ahsante.

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOHN F. NZILANYINGI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara ya njia nne kutoka Mjini – Usagara na kutoka Mjini – Kisesa?

Supplementary Question 2

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Balili – Mugeta, tayari upembuzi yakinifu umeshafanyika, na wewe Naibu Waziri unaijua, na iko kwenye Ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi na juzi Mwenezi ametoka kwenye Jimbo la Bunda Mjini na wananchi wamemwomba kuhusu barabara hii. Nataka kujua ni lini itajengwa kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, tukishafanya usanifu inakuwa ndiyo hatua za mapema ambazo Serikali sasa tunakuwa tumejua gharama ya hiyo barabara. Nimhakikishe Mheshimiwa Mbunge kwa maana ya kufanya usanifu, maana yake Serikali imeweka hiyo barabara kwenye mpango, kujenga kwa kiwango cha lami. Bajeti yetu tunaanza kesho, kwa hiyo nimhakikishe Mheshimiwa avute subira tuone kwenye bajeti tutakuja na nini kuhusu hiyo barabara. Ahsante