Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Edibily Kinyoma Kazala

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kasulu Vijijini

Primary Question

MHE. EDIBILY K. KINYOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Uvinza – Kasulu na Makere – Nyarugusu Kitanga kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. EDIBILY K. KINYOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hizi ni ahadi ya Mheshimiwa Rais, lakini pia Mheshimiwa Naibu Waziri amekuwa Mkurugenzi kwenye Halmashauri yetu anafahamu umuhimu wa hizi barabara. Je, Serikali haioni haja ya kutenga fedha kwenye hii bajeti kuhakikisha barabara hizi zinajengwa kwa kiwango cha lami?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia swali la pili, barabara hizi zimepita karibu na SGR, mahali ambapo SGR inajengwa kuelekea Burundi. Je, Serikali haioni iko haja ya kuzijenga barabara hizi kwa haraka ili wananchi waweze kunufaika na fursa za SGR kabla SGR haijamalizika kujengwa? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda nianze na Barabara ya Uvinza - Kasulu. Barabara ya Uvinza - Kasulu nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge, kimsingi ndiyo tunayoita T Number Nine ambayo inatoka Tunduma – Mpanda – Uvinza - Kasulu hadi Nyakanazi. Nakubaliana naye kwamba ni kipande hicho tu ambacho kwa sasa kinatafutiwa fedha ili kiweze kujengwa na tukamilishe barabara yote Nyakanazi – Kasulu - Mpanda, Sumbawanga hadi Tunduma. Kwa hiyo, nakubaliana na wewe na Serikali inalijua hilo. Kwa hiyo, tunafanya kila jitihada tutafute fedha kuanza kuijenga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Barabara ya Makere - Nyarugusu kwenda Kitanga, Mheshimiwa Mbunge anakubaliana nami kuwa hiyo barabara ilikuwa inahudumiwa na wenzetu wa TARURA, ndiyo imepandisha hadhi na nadhani ndiyo kwanza tunataka tuitengeneze iwe katika mfumo wa TANROADS, wakati tunaendelea kutafuta fedha ya kuisanifu ili kwa kweli iweze kujengwa kwa kiwango cha lami, kwa sababu inaenda sambamba pia na SGR, pia inaenda mpakani, nchi ya Burundi. Kwa hiyo, tunalifahamu hilo, ndiyo maana tumeipandisha na tunaitafutia fedha kuisanifu ili tuweze kuijenga kwa kiwango cha lami. Ahsante

Name

Yustina Arcadius Rahhi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. EDIBILY K. KINYOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Uvinza – Kasulu na Makere – Nyarugusu Kitanga kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 2

MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali itaanza kujenga lini barabara ya Karatu - Mbulu kipande cha kilometa 76, kwa kuwa iko kwenye Ilani, lakini vilevile ni ahadi ya viongozi? Ahsante sana.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom - Sibiti hadi Lalago – Maswa ni barabara ambayo ilitakiwa ijengwe yote, lakini baada ya kusitisha ule mpango, tumeigawa katika vipande vitatu ambao tumeshaanza kuijenga. Tumeanza Mbulu hadi Garbabi - Labay hadi Haydom. Sasa hivi tunaenda Nkoma kwenda Lalago. Kwa hiyo, tutakuja baada ya kukamilisha hivyo vipande vitatu, utaratibu utakaofuata sasa itakuwa ni kujenga Mbulu kwenda Karatu. Ahsante.