Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ester Edwin Malleko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza upatikanaji wa mbegu bora na kwa bei nafuu nchini?
Supplementary Question 1
MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu mazuri na maswali mawili ya nyongeza.
Swali la kwanza; Serikali ina mkakati gani basi wa kuhakikisha wananchi hasa wa vijijini wanapatiwa mbegu bora kwa wakati?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; nini mkakati wa Serikali katika kudhibiti mbegu fake ambazo zimekuwa ni changamoto kubwa sana kwa wakulima wanapata hasara?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na ninamshukuru Mheshimiwa Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Kilimanjaro, kwa maswali madogo ya msingi yenye maslahi mapana kwa wakulima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimthibitishie tu kwamba moja, Serikali katika mkakati wetu wa kupeleka mbegu vijijini ni kuhakikisha sasa hivi kwamba mbegu zinapatikana kabla ya msimu, lakini la pili; Serikali kupitia TFRA tumesajili mawakala na wasambazaji wa mbegu na tumeongeza idadi ya wasambazaji kwenda kule vijijini, na sasa hivi tunataka walau karibu katika kila kijiji kuwe na wakala ambapo mwananchi wa kawaida anaweza kufika na kupata mbegu kwa urahisi.
Kwa hiyo, hiyo ni sehemu ya mikakati ambayo Serikali tunaifanya sasa hivi ili kuhakikisha mbegu zile zinawafikia wakulima kwa urahisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu udhibiti wa mbegu fake, sisi kutumia mamlaka yetu ya TOSCI ambao ndio wathibitishaji wa hizi mbegu na ndio ambao wanadhibiti matumizi ya mbegu, wamekuwa na jukumu moja la kufanya patrol za mara kwa mara lakini pili, kwa wale ambao wamekuwa wakikiuka taratibu, moja tunawanyang'anya leseni za kufanya biashara ya mbegu hapa nchini, lakini pili tunawafungulia mashtaka katika mahakama zetu, na wale wanaokutwa na hatia kuna fidia pamoja na hatua nyingine za kisheria ambazo zimekuwa zikichukuliwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hiyo ni sehemu ya jitihada ambazo Serikali tumeendelea kuzifanya, lakini tutaendelea kuongeza elimu bora kwa wananchi ikiwemo za kutumia zile code maalum ili mwananchi anaponunua mbegu ile anatuma kwenye ile code maalum ambayo ataweza kuambiwa mbegu hii ni fake, imezalishwa wapi ama imepakiwa sehemu gani, na mtu gani ambaye anasambaza hiyo mbegu. Kwa hiyo, hizo ni taratibu ambazo tunataka tumsaidie mkulima na ndio maelekezo ya Serikali na sasa hivi tupo katika kuyatekeleza, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved