Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Christina Solomon Mndeme
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CHRISTINA S. MNDEME aliuliza: - Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha inawafikia Wanawake wote wenye uhitaji wa Mikopo katika Mkoa wa Tabora?
Supplementary Question 1
MHE. CHRISTINA S. MNDEME: Mheshimiwa Mwenyekiti, Ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Ninayo maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa Serikali imekuwa na mpango mzuri wa kuwawezesha wananchi kiuchumi na hususan wanawake wa Mkoa wa Tabora. Tunampongeza sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwa mikopo hiyo imekuwa ikileta tija kwa wanawake wanaokopeshwa.
(a) Je, Serikali inapango gani wa kutoa elimu ya fedha na ujasiriamali kwa wanawake wanaopata mikopo kwa kuwafuata katika maeneo yao walipo?
(b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuwa na mfumo mzuri wa ufuatiliaji wa matumizi ya mikopo hiyo ili kufahamu changamoto walizopitia na wanazopitia wanawake wakati wa kutumia mikopo hiyo ambayo inaweza kuathiri urejeshaji wa mikopo waliyochukua, na hasa wanawake wa Mkoa wa Tabora?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge Dkt. Christina Solomon Mndeme amesema, ni kweli kwamba mikopo hii imekuwa na tija kubwa sana kwa makundi maalumu, wakiwemo wanawake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa kutambua kwamba wako wanawake ambao wako maeneo ya vijijini, na ambao mara nyingine ni ngumu kufika katika Makao Makuu ya Halmashauri, tumeunda kamati za mikopo kuanzia ngazi za kata na halmashauri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tumeendelea kuwafundisha Maafisa Watendaji wa Kata, na tunaendelea pia kuwafundisha Maafisa Watendaji wa Vijiji ili katika maeneo husika waweze kuwa msaada kwa kutoa elimu, hamasa na kuwezesha vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kuandika maandiko sahihi ya kibiashara na waweze kupata mikopo hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja hao, Maafisa Maendeleo ya Jamii wamekuwa mara kwa mara wakifanya huduma mkoba kwa kwenda kule maeneo ya vijijini na kukutana na vikundi hivi na kuendelea kuelimisha. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mpango huo unaendelea na Serikali itahakikisha inaendelea kufanya hivyo ili kuongeza uwezo wa vikundi kupata mikopo hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili, wakati tunafanya mafunzo hayo pia tunafanya tathmini ya ufanisi wa biashara ambazo vikundi hivyo vinaendesha kupitia mikopo ya 10% na kuona maeneo ambayo yana changamoto na kuwasaidia ili wawe na mafanikio na waweze kuwa na urejeshaji mzuri. Suala hili tutaendelea kulifanya ili kuhakikisha mikopo ya 10% inakuwa na ufanisi mkubwa zaidi.
Name
Tinnar Andrew Chenge
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CHRISTINA S. MNDEME aliuliza: - Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha inawafikia Wanawake wote wenye uhitaji wa Mikopo katika Mkoa wa Tabora?
Supplementary Question 2
MHE. TINNAR A. CHENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Ninakushukuru. Kwa kuwa ni Sera ya Serikali ya Kuwainua Wanawake Kiuchumi kupitia mikopo ya 10%, je, Serikali ina mpango gani wa kufikisha elimu juu ya mikopo yenye riba nafuu inayotolewa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii kwa wanawake wa vijijini Mkoa wa Simiyu?
MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, sijasikia vizuri.
MWENYEKITI: Mheshimiwa, ni kuhusu mikopo ya wanawake Simiyu, majibu kwa ufupi.
MHE. TINNAR A. CHENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mpango gani wa kufikisha elimu ya mikopo yenye riba nafuu inayotolewa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii kwa wanawake wa vijijini wa Mkoa wa Simiyu? Ninashukuru.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI pamoja na Wizara ya Maendeleo ya Jamii tunafanya kazi kwa pamoja katika maeneo ya makundi maalum.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge Wizara ya Maendeleo ya Jamii inaendelea pia kuwafikia wanawake na makundi yale ambayo yanahitaji kupata mikopo hiyo kutoa elimu juu ya upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu. Kwa hiyo, Ofisi ya Waziri Mkuu tumelichukua hilo. Tutakaa kwa karibu zaidi na Wizara ya Maendeleo ya Jamii ili kuendelea kuboresha mbinu za kuwafikia akina mama na kujua kwamba kuna fursa za mikopo hiyo.
Name
Neema Peter Majule
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CHRISTINA S. MNDEME aliuliza: - Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha inawafikia Wanawake wote wenye uhitaji wa Mikopo katika Mkoa wa Tabora?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. NEEMA W. MAJULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Swali langu ni hili hapa. Je, ni vipi na ni lini Serikali itafanya impact assessment kuona matokeo ya mikopo hii inayotolewa kwa wanawake inawa-transform kweli wanawake? Yaani inawabidisha kabisa wanawake; au tutakumbana na njia nyingine mbadala, labda badala ya kutoa hii mikopo kidogo kidogo kwa kila mwanamke labda tuje na kujenga viwanda ambavyo vitaweza kuajiri vijana wanawake na watu wenye ulemavu, ni lini itafanya impact assessment ili tuone matokeo?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Dkt. Neema ameongea jambo la muhimu sana la kufanya impact assessment kuona namna ambavyo mikopo hii imesaidia kuwakomboa akina mama, vijana na watu wenye ulemavu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kufanya tathmini, na tuna ushahidi wa maendeleo ya biashara hizi kwa baadhi ya vikundi. Viko vikundi ambavyo vilianza na mikopo ya milioni tano kwa mfano, lakini wakakuza biashara zao na kukopa shilingi milioni 50, shilingi milioni 60 na kuendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaona kuna mwendelezo mzuri wa baadhi ya vikundi ku-graduate kutoka kukopa kidogo kidogo na kufanya biashara ndogo na baadaye wanaanzisha viwanda vya kuchakata bidhaa mbalimbali kama za kilimo na bidhaa nyingine. Kwa hiyo, tunaamini kwamba mikopo hii inaleta tija.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wazo la kufanya impact assessment tumelichukua ili tujue, tufanye kwa ujumla wake tangu tumeanza mpaka sasa tuweze kuona mwelekeo wa tija katika mikopo hii na kuweka mipango mizuri zaidi ya kuboresha tunakoelekea mbele. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved