Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mgore Miraji Kigera
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Musoma Mjini
Primary Question
MHE. MGORE M. KIGERA aliuliza: - Je, Serikali imefikia wapi kuhusu mwekezaji aliyeonesha nia ya kuwekeza Hoteli ya New Musoma ambayo ni alama ya Mji na Mkoa wa Mara?
Supplementary Question 1
MHE. MGORE M. KIGERA: Mheshimiwa Spika, nashukuru, kwanza napenda kutoa pongezi na shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa majibu mazuri ya kuonesha dhamira ya dhati ya kuweza kufufua ya New Musoma Hotel. Nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeonesha nia ya kuanzisha Tourism Corridor between Serengeti National Park na Lake Victoria. Je, haioni sasa umuhimu wa kuharakisha mchakato huu ili kuweza kupata mwekezaji huyo kwa uharaka. Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Mipango na Uwekezaji aliwaahidi wananchi wa Jimbo la Musoma Mjini kufikia Julai, mwekezaji huyu atakuwa amekabidhiwa hoteli hiyo. Ni lini sasa Serikali itaona umuhimu wa kulifanya hili kwa uharaka?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; kupitia hoteli ya New Musoma, itaweza kuleta watalii pamoja na wawekezaji kwa uharaka. Tuna uwanja wetu wa ndege wa Musoma, mpaka sasa haujaweza kuanza kufanya kazi. Je, Serikali inatuambia nini Wananchi wa Musoma na Mkoa wa Mara, uwanja huo lini utaanza kufanya kazi rasmi? (Makofi)
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mgore Kigera, kwa jinsi ambavyo anafuatilia maendeleo ya wananchi wa Musoma, wilaya au mkoa ambao ni muhimu kwa Taifa letu.
Mheshimiwa Spika, kwanza, tunatambua umuhimu huo ndiyo maana tumeshaanza mchakato Serikalini kuifufua hoteli hiyo, kushirikisha sekta binafsi, kwa sababu tunatambua kwamba pale Musoma kuna ziwa, kuna shughuli za uvuvi na usafirishaji majini, pale Musoma kuna hifadhi kwa maana ya kwamba watalii wanahitaji kupata hoteli nzuri ambayo ni ya kisasa, pale Musoma kuna madini, lakini pale Musoma kwenye Mkoa huo ndipo anapotoka baba wa taifa. Kwa hiyo, watu wengi sana wangependa kwenda katika mkoa huo.
Mheshimiwa Spika, tayari tumeshaanza mchakato huo na mhusika mmojawapo mwekezaji binafsi ambaye ameonesha nia ameshapatikana. Tutakwenda kwa ushauri wake alioutoa, ambao ndio wa Kibunge, kuongeza kasi ya majadiliano ili tufike hatima nzuri, hatimaye hoteli hii muhimu iweze kuanza kufanya kazi.
Mheshimiwa Spika, swali la pili; ameuliza kwamba hoteli hii itategemea pia iweze kupokea wateja au watu wanaokuja kwenye shughuli mbalimbali ambao kimsingi tunakusudia moja ya usafiri utakaotumika ni uwanja wa ndege, anataka kufahamu ni lini utakamilika.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali hii ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeonesha kutambua na kuthamini umuhimu wa kuboresha Uwanja wa Ndege wa Musoma ndio maana imeidhinisha shilingi bilioni 36 na ujenzi uko 67%.
Mheshimiwa Spika, wiki iliyopita Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Profesa Mbarawa, alinituma hapa nitoe route mpya ya ndege zetu na miongoni mwa maeneo ambayo aliyatolea maelekezo ni pamoja na Uwanja wa Ndege wa Musoma pamoja na Shinyanga ambapo mwezi huu tunakusudia kuanza majaribio ya ndege kwenye viwanja viwili, Musoma pamoja na Shinyanga. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nimsihi Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wengine kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Dkt. Samia, kwa sababu anazidi kuleta tabasamu kwa wananchi wake. (Makofi)
Name
Esther Nicholas Matiko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Tarime Mjini
Primary Question
MHE. MGORE M. KIGERA aliuliza: - Je, Serikali imefikia wapi kuhusu mwekezaji aliyeonesha nia ya kuwekeza Hoteli ya New Musoma ambayo ni alama ya Mji na Mkoa wa Mara?
Supplementary Question 2
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kuweza kunipatia fursa na mimi kuuliza swali.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Tanzania tunatarajia kunufaika na uwepo wa AFCON na ukuaji wa utalii, na kwa kuwa wageni ambao watakuja kipindi cha AFCON watahitaji hoteli zenye hadhi ya nyota nne mpaka tano wengine.
Serikali ina mkakati gani wa haraka wa kuweza kufufua au kutafuta wawekezaji kwenye hoteli za umma ambazo zimetelekezwa kwa muda mrefu kama vile Motel Agip na Embassy ili ziweze kuongeza malazi, ajira na mapato ya taifa kuliko kuendelea kuwa liability kwa Taifa? (Makofi)
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Esther Matiko, aliyeuliza kwa ujumla hoteli mbalimbali za Serikali.
Mheshimiwa Spika, mimi kimsingi, kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi, nitajikita kwenye miradi iliyopo kwenye sekta yetu. Kama ambavyo nimeshaanza kumjibu Mheshimiwa Mgore, tunatambua maeneo mbalimbali, kwanza, kwa ajili ya kuongeza ajira, ukifufua hoteli unaongeza ajira kwa wananchi, lakini pili, unaimarisha utalii. Kwa maeneo ambayo ni ya kimkakati ambapo AFCON inakwenda kutumika maana yake pia inasaidia kuongeza accommodation, wananchi waweze kupata mahali au washiriki kwenye kombe hilo, waweze kushiriki.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ametuongezea msukumo mkubwa zaidi ya kutushauri na kutukumbusha Serikalini ili tuendelee kuona umuhimu wa kuweza kufufua maeneo hayo kwa maslahi ya Watanzania wote.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved