Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Moses Charles Bujaga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Sumve
Primary Question
MHE. MOSES C. BUJAGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Malya – Nyambiti (kilometa 58) ili kuboresha usafirishaji katika Jimbo la Sumve?
Supplementary Question 1
MHE. MOSES C. BUJAGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, barabara hii ya Fulo - Nyambiti – Malya ilitakiwa kukamilika huo upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kufikia mwezi wa Aprili, 2026. Ningependa kufahamu ni kwa nini kazi hiyo haijakamilika mpaka sasa? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, barabara hii kwa sasa iko katika hali mbaya sana na ndiyo inayobeba uchumi wa Jimbo la Sumve, minada ya Bungulwa, usafirishaji wa mazao kama dengu na pamba ambayo ndiyo msimu wa sasa hivi utakuwa ni changamoto. Serikali ina mpango gani kuhakikisha barabara hii inapitika, ili kurahisisha usafirishaji wa mazao na usafiri wa wananchi? (Makofi)
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI K.n.y. WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Moses Charles Bujaga, Mbunge wa Sumve, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, awali napenda kumpongeza kwa jinsi ambavyo amekuwa ni mtu wa shukrani ya kutambua kazi nzuri ambayo inafanywa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye eneo lake, lakini pili, amekuwa ni mfuatiliaji makini, kwa huu muda mfupi wote tunashuhudia, anavyopigania barabara za jimbo lake na hata za mkoa wake kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika, ameuliza kwa nini haijakamilika katika muda uliokuwa umepangwa; moja, mhandisi mshauri alikuwa ameshakamilisha ile kazi, lakini kama unavyofahamu, mahitaji yanazidi kuongezeka. Timu ya wataalam ikapitia na kubaini kwamba kuna mambo mengine ambayo yakiongezwa, yatakuwa na maslahi mapana zaidi kuliko walivyofikiria pale awali na kimsingi jambo hili ni jambo jema kwa sababu pengine barabara ya awali ilikuwa inakusudiwa, ilitazamiwa kwa mahitaji ya pale mwanzoni.
Kwa hiyo, wataalamu wakaona iko haja kufanya maboresho, ili barabara itakayofikiwa kuamuliwa kujengwa, iendane na ndoto na matamanio ya yeye Mbunge, wananchi na Taifa letu kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika, nimwombe awe na subira, kwa sababu baada ya hatua hii sasa, tumemwongezea mkandarasi muda, angalau mpaka kabla ya mwezi wa Agosti au kabla ya mwaka huu haujaisha ili kazi hii iwe imekamilika.
Mheshimiwa Spika, la pili; ameuliza kwamba barabara hii imekuwa ni mbovu ambayo kimsingi sisi Serikali tunakubaliana na yeye na tunampa pole kwa changamoto hiyo, kawaida barabara hii itakiwa ifanyiwe ukarabati mara mbili kwa maana mwezi wa 10 pamoja na mwezi Mei mpaka Juni. Mwaka jana mwezi wa 10 ukarabati mzuri ulifanyika, sasa kipindi kama hiki ambacho wakulima na wananchi wanakusudiwa kusafirisha mazao mbalimbali kama vile pamba, dengu na mazao mengine barabara hiyo kweli ni mbovu.
Mheshimiwa Spika, tayari taratibu zimeshaanza kufanyika ili mkandarasi huyu sasa aingie kazini hivi karibuni na namwelekeza kwa Niaba ya Waziri wa Ujenzi amenituma nimwelekeze Meneja wa TANROADS ili alisimamie jambo hili mkandarasi huyo aingie kazini, aanze kufanya kazi na aboreshe barabara hii ili wananchi wa Sumbe na Mkoa wa Mwanza na maeneo jirani kwa ujumla waweze kunufaika na barabara hii na kujenga uchumi wao.
Name
Suma Ikenda Fyandomo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MOSES C. BUJAGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Malya – Nyambiti (kilometa 58) ili kuboresha usafirishaji katika Jimbo la Sumve?
Supplementary Question 2
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Rungwe kuna barabara ya muhimu sana inayotoka Kiwila, Kinyala inapita Isangati inatokea Mbalizi. Barabara hiyo wananchi wanateseka sana namna ya kusafirisha mazao yao na kusafiri wao wenyewe hasa wanawake.
Mheshimiwa Spika, je, ni lini barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI K.n.y. WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Suma Fyandomo, Mbunge kutoka Mkoani Mbeya anayewakilisha kina mama kwa jinsi anavyowapigania Wananchi wa Mkoa wa Mbeya wakiwemo wa Rungwe, wakiwemo wa Kyela, Mbozi, Chunya na maeneo mengine yote na kimsingi barabara hii sisi kama Serikali tunatambua umuhimu wake.
Mheshimiwa Spika, nimwombe Mheshimiwa Suma Fyandomo pamoja na Wabunge wa majimbo wa maeneo hayo na wananchi kwa ujumla wawe na subira, Serikali inatambua umuhimu wa barabara hii na maeneo mengine ni muhimu yakajengwa kiwango cha lami, lakini kwa sasa sungura ni mdogo tujipe muda wakati utafika itajengwa na watafurahia.
Name
Simon Songe Lusengekile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busega
Primary Question
MHE. MOSES C. BUJAGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Malya – Nyambiti (kilometa 58) ili kuboresha usafirishaji katika Jimbo la Sumve?
Supplementary Question 3
MHE. SIMON S. LUSENGEKILE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Tunayo barabara ya kutoka pale Nyashimo kwenda Dutwa Wilaya ya Bariadi kupitia pale Maliri, Shigala, Ngasamo pamoja na Dutwa yenyewe inayounganisha wilaya mbili na tumekuwa tukiahidiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.
Je, ni lini Serikali sasa itaanza ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami kwa ajili ya uchumi wa hizi wilaya mbili?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI K.n.y. WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi swali la Mheshimiwa Songe ambaye anaielezea barabara hiyo yake muhimu na nipende kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge pamoja na Wabunge wengine wote kwa sababu naamini eneo hili ni eneo nyeti sana Serikali inatambua umuhimu wa barabara katika uchumi wa Taifa lake na kwa sasa kama ambavyo Waziri wa Ujenzi amesimama mara kadhaa tupo kwenye mchakato Serikalini, kwanza ya kutambua wakandarasi ambao walikwishaanza kazi wamesimama, wakandarasi ambao walikwishaanza kazi walisimama na ambao pengine mikataba yao hawajisainiwa lakini pia maeneo mengine ambayo bado hayajasainiwa na yanayotakiwa kutangazwa.
Mheshimiwa Spika, niwahakikishieni mlimsikia mwenyewe Mheshimiwa Waziri Mkuu akizungumza hapa na naomba tuwe na subira Waheshimiwa Wabunge. Barabara hizi baada ya kuwa tumeshafanya kazi nzuri ya kusimamia uchaguzi wenyewe kwa hela zetu kujenga Daraja la Busisi, kujenga SGR, kujenga Bwawa la Mwalimu Nyerere na kufanya mambo mengine mengi makubwa ninayo hakika Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anakwenda kujenga barabara mbalimbali kwenye nchi hii zikiwemo hata zile za kule Mufindi ambazo tunazipigania kila wakati.
Name
Zacharia Paulo Issaay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Primary Question
MHE. MOSES C. BUJAGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Malya – Nyambiti (kilometa 58) ili kuboresha usafirishaji katika Jimbo la Sumve?
Supplementary Question 4
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Barabara ya Mlima Magara katika Jimbo la Mbulu Mjini barabara yenye jiografia ngumu sana, na kwa kuwa mkandarasi aliyekuwa anajenga zege katika Mlima Magara amesimama kwa muda wa zaidi ya mwaka moja; ni lini mkandarasi atarudi site ili akamilishe zege katika Mlima Magara?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI K.n.y. WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia barabara yake muhimu ambayo kimsingi mkandarasi alikuwa site kama alivyoeleza amesimama.
Mheshimiwa Spika, mara tutakapokamilisha taratibu za fedha tukishamlipa mkandarasi huyo atarejea kufanya kazi na wewe Mheshimiwa Mbunge na wananchi tunaomba muwe na subira kwa kipindi hiki.
Name
Josephine Tabitha Chagulla
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MOSES C. BUJAGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Malya – Nyambiti (kilometa 58) ili kuboresha usafirishaji katika Jimbo la Sumve?
Supplementary Question 5
MHE. JOSEPHINE T. CHAGULA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona, barabara inayotoka Kahama kupitia Nyang'hwale mpaka Busisi ni barabara muhimu sana kwa biashara na uchumi wa Mkoa wa Geita. Je, ni lini Serikali itajenga barabara hii kwa kiwango cha lami?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI K.n.y. WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, Serikali inayo dhamira ya kuhakikisha wananchi wanaopita kwenye barabara hiyo inayotokea Kahama wanaboreshewa barabara hiyo, lakini kwa sasa kwa kuwa fedha hazipo tunaomba wananchi wavumilie, tunaendelea na mchakato Serikalini pale itakapokuwa tayari Serikali itakwenda kujenga kwa kiwango cha lami.
Name
Esther Lukago Midimu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MOSES C. BUJAGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Malya – Nyambiti (kilometa 58) ili kuboresha usafirishaji katika Jimbo la Sumve?
Supplementary Question 6
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, barabara ya kutoka Bariadi kwenda Lamadi ina hali mbaya sana, ina mashimo na mabonde imebomoka bomoka. Je, ni lini Serikali itafanya ukarabati wa barabara hiyo?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI K.n.y. WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi namwelekeza Meneja wa TANROADS wa Mkoa huo wa Simiyu aende atazame barabara ambayo imelalamikiwa na Mheshimiwa Mbunge ili atazame kiwango cha uharibifu na kisha kuweza kuweka mpango wa namna bora ya kuweza kuikarabati ili Serikali na wananchi waendelee kunufaika.
Name
Salma Rashid Kikwete
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Mchinga
Primary Question
MHE. MOSES C. BUJAGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Malya – Nyambiti (kilometa 58) ili kuboresha usafirishaji katika Jimbo la Sumve?
Supplementary Question 7
MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Barabara yetu ya Milola - Kiwawa, Milola - Kutwa itajengwa kwa kiwango, mimi sihitaji lami mimi nahitaji changarawe na hizi barabara ni muhimu sana na hizi barabara umuhimu wake mkubwa ni sehemu ambayo inazalisha ufuta kwa kiwango kikubwa sana na ukubwa wa barabara hii ni kilometa sita tu. Je, lini Serikali itatupatia pesa kujenga barabara hizi?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI K.n.y. WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi ninamwelekeza Meneja wa TANROADS aende akaone eneo hilo la kilometa sita ambalo limelalamikiwa au limeombewa na Mheshimiwa Mbunge kwamba lina usumbufu na hivyo linahatarisha biashara ya ufuta pamoja na wananchi kupita kwenye maeneo hayo na kwa msingi Mbunge anatimiza jukumu la msingi la Kibunge la kuishauri na kuisimamia Serikali na sisi Serikali hii ya Mheshimiwa Dkt. Samia wakati wote tumesisitizwa kuwa wasikivu kwa sauti za Wabunge na mara baada ya kujua mahitaji halisi basi Serikali itachakata na kuwa namna bora kuweza kufanyia kazi ombi la Mheshimiwa Salma Kikwete, Mbunge kama alivyoomba.