Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Salum Khamis Salum
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Meatu
Primary Question
MHE. SALUM K. SALUM aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza utekelezaji wa Mradi wa Barabara ya Nkoma – Lalago kilometa 65?
Supplementary Question 1
MHE. SALUM K. SALUM: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini tu kumkumbusha kwamba barabara hiyo imewekwa kwenye ilani safari ya tatu hii ilani tatu na siku zote inakosa fedha. Sasa ni muhimu mkajua umuhimu wa barabara hiyo kusudi bajeti hii itengewe fedha na mkandarasi aanze.
Mheshimiwa Spika, pili, barabara hiyo inakutukutanisha sisi Mkoa wa Simiyu pamoja na Mkoa wa Singida kwa Daraja kubwa la Mto Sibiti, Daraja la Sibiti lilivyojengwa lilikuwa lina kilometa 24 za lami ambazo contractor CHICO alishapewa mkataba huo, kwa hiyo, tunaiomba tena Wizara impe fedha mkandarasi CHICO kusudi ajenge kilometa 24 ambazo kilometa zingine zitakuwa kwa Mkoa wa Singida na zingine Mkoa wa Simiyu.
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI K.n.y. WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi nampongeza Mheshimiwa Salum Khamis Salum kwa kuendelea kufuatilia miradi ya kimkakati ikiwemo barabara hii muhimu sana kwa uchumi na maisha ya wananchi wake.
Mheshimiwa Spika, kimsingi kama alivyosema barabara hii imekuwa ikiahidiwa mara kadhaa kwenye Ilani ya CCM, lakini pamoja na kuahidiwa mara kadhaa kwenye ilani za huko nyuma ni wajibu wetu yeye mwenyewe Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wote kuweza kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuamua sasa kwanza kuijenga, kitendo cha kusaini mkataba na kampuni ya CCECC ni dhamira ya dhati kwamba Serikali sasa imeamua inaenda kuijenga.
Mheshimiwa Spika, na kwa sasa kama ambavyo tumesema kwenye majibu ya msingi Serikali baada ya kuwa imeshasini mkataba inafanya taratibu za kutafuta fedha Serikalini.
Mheshimiwa Spika, nimwombe Mheshimiwa Mbunge pamoja na wananchi kwa ujumla wawe na subira dhamira ya Serikali ya kuijenga barabara hii kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge mara kwa mara anakumbushia iko pale pale, subira yavuta kheri, tutaifikia barabara hiyo kuijenga vizuri na wao watafurahia.
Name
Kangi Alphaxard Lugola
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwibara
Primary Question
MHE. SALUM K. SALUM aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza utekelezaji wa Mradi wa Barabara ya Nkoma – Lalago kilometa 65?
Supplementary Question 2
MHE. KANGI A. LUGOLA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Barabara ya kutoka Busambara hadi Mugara - Iramba zaidi ya miaka 10 tuliomba iingizwe kwenye huduma ya TANROADS na tunaambiwa mchakato unaendelea zaidi ya miaka 10.
Sasa je, ni lini mchakato huu utakamilika kwa sababu barabara hii inaendelea kuharibika sana na mpaka sasa magari hayapiti? Ahsante.
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI K.n.y. WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Kangi Lugola kwa kukumbushia ombi lake muhimu, ninaomba awe na Subira, wakati Serikali inaendelea na mchakato wa kina wa kuona namna bora ya kuweza kuihudumia barabara hiyo, na mara baada taratibu zitakapokamilika Serikalini basi ombi la Mheshimiwa Kangi Lugola litakwenda kukamilika.
Name
Ramadhani Hamza Singano
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bumbuli
Primary Question
MHE. SALUM K. SALUM aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza utekelezaji wa Mradi wa Barabara ya Nkoma – Lalago kilometa 65?
Supplementary Question 3
MHE. RAMADHANI H. SINGANO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Barabara ya Mombo – Soni - Lushoto ni barabara ya kimkakati kwa majimbo matatu. Ni lini Serikali itaona umuhimu wa kuipanua barabara hii ili kukidhi haja katika eneo hili?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI K.n.y WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge pia kwa kufuatilia barabara yake ambayo ni muhimu kwa sababu barabara ndiyo mishipa ya uchumi wa nchi yetu, lakini muombe awe na subira. Tutaendelea na mchakato Serikalini itakapokuwa tayari tutakwenda kuikamilisha na hivi ndivyo tunakwenda Serikalini kwa vipaumbele, baada ya kumaliza hatua moja tunakwenda hatua nyingine barabara moja tunakwenda barabara nyingine.
Name
Morris Joseph Makoi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Mjini
Primary Question
MHE. SALUM K. SALUM aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza utekelezaji wa Mradi wa Barabara ya Nkoma – Lalago kilometa 65?
Supplementary Question 4
MHE. MORRIS J. MAKOI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, Barabara ya Kagongwa – Igusule - Mwamara mpaka Nzega imeshajengwa mpaka tabaka la tatu kutoka Kagongwa kwenda Igusule kilometa 18.3 kilichobaki ni kuwekwa lami kipande hicho cha kilometa 18.3. tukikiacha kitaharibika.
Mheshimiwa Spika, sasa Serikali ina mpango gani wa kukamilisha uwekaji wa lami kilometa 18.3 kutoka Igusule kwenda Kagongwa ili kuokoa thamani ya fedha iliyotumika hadi sasa?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI K.n.y WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Morris kwa kukumbushia barabara yake muhimu kama ambavyo nimesema kwenye majibu ya msingi, Serikali inayo dhamira ya dhati na inawahakikishia Wabunge wote ikiwemo Mheshimiwa Mbunge huyu miradi yote ambayo tumekwisha kuianza tutakwenda kuikamilisha na ile ambayo tunakusudia kuianza Serikali inakwenda kuikamilisha.
Mheshimiwa Spika, naomba awe na subira kwa kuwa tumeshaonesha nia, Serikali imekwisha anza ujenzi hata kipande hicho Serikali itakwenda kukikukamilisha ili kuwaweza kusikiliza kilio na maombi ya wananchi wa eneo hilo kama ambavyo imewasilishwa na Mheshimiwa Mbunge leo.
Name
Emmanuel Peter Cherehani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ushetu
Primary Question
MHE. SALUM K. SALUM aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza utekelezaji wa Mradi wa Barabara ya Nkoma – Lalago kilometa 65?
Supplementary Question 5
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Spika, ahsante, barabara inayotoka Mkunze inaenda Iponyang’olo - Ilamba, Igwamanoni inapakana na wenzetu wa Masumbwe ni barabara ambayo imepanda kwenda TANROADS leo miaka minne, lakini haijawahi kutengewa fedha na wala hawajafika hata kuikagua. Ni nini mkakati wa Serikali juu ya barabara hiyo?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI K.n.y WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa uvumilivu wake pamoja na kwamba anasema barabara yake haikutengewa fedha na kwa kweli anafuatilia sana maendeleo ya jimbo lake, wilaya yake na sekta zote.
Mheshimiwa Spika, nimwombe Mheshimiwa Cherehani vuta subira. Serikali hii imefanya mambo mengi na makubwa zaidi haitashindwa kujenga barabara za nchi hii ikiwemo ya kwako. Tujipe muda hatua kwa hatua, tutaifikia barabara yake na yeye atafurahi pamoja na wananchi kama ambavyo tumekwisha fanya kwenye maeneo mengine ya maji, umeme pamoja na sekta zingine ndani ya jimbo lako.
Name
Ibrahim Mohamed Shayo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Mjini
Primary Question
MHE. SALUM K. SALUM aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza utekelezaji wa Mradi wa Barabara ya Nkoma – Lalago kilometa 65?
Supplementary Question 6
MHE. IBRAHIM M. SHAYO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mheshimiwa Naibu Waziri umekuwa ukiniambia kila siku tarehe 01 Juni, mkandarasi ataingia site kuhusu barabara ya Mailisita kuelekea Kiboroloni ya njia nne. Je, ni lini unawaambia wananchi wa Moshi Mjini mkandarasi ataingia site?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI K.n.y WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Shayo kwa jinsi ambavyo anakumbushia barabara hii. Endelea kuvuta subira Mheshimiwa Shayo, tunakamilisha taratibu za kifedha ndani ya Serikali kama ambavyo Serikali hii imefanya mengi kwenye Jimbo la Moshi na wewe unafahamu kwenye uwanja wa ndege tumepeleka mabilioni pale, nataka nikuhakikishie hata hii vuta subira tutakwenda kufika na wananchi wa Moshi watafurahia.