Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Alan Thomas Mvano

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kakonko

Primary Question

MHE. ALAN T. MVANO aliuliza: - Je, lini Mkandarasi atakamilisha kuchimba na kujenga kisima cha maji katika Kijiji cha Kihomoka kama ilivyo kwenye mkataba wake?

Supplementary Question 1

MHE. ALAN T. MVANO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali na jitihada hizo, ninaamini Waziri atakuwa tayari kuongozana na mimi kwenda Kakonko ili aweze kujionea hali ya upatikanaji wa huduma ya maji ilivyo, lakini pamoja na hayo nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; Katika Kijiji cha Kihomoka wapo wananchi wanaishi eneo linaitwa Nabulilije na wanatembea kilometa 10 kufuata huduma ya majisafi na salama. Sasa ni upi mpango wa Serikali wa dharura kuhakikisha kwamba wananchi hawa sasa wanapata huduma hiyo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Wafanyakazi wa Serikali, wa RUWASA pamoja na Mamlaka ya Maji wamekuwa wakipata shida sana kutembea katika Wilaya ya Kakonko katika kushughulikia changamoto za maji. Ni upi mpango wa Serikali kuhakikisha sasa wanapelekewa gari ili waweze kufanya shughuli zao vizuri na wananchi wapate huduma ya maji? Ahsante sana.

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninakubaliana na ombi la Mheshimiwa Alan Thomas Mvano, Mbunge wa Kakonko. Niko tayari kuongozana naye kwenda Kakonko, ili kujionea hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza Sana Mheshimiwa Mbunge kwa juhudi na ufuatiliaji wa miradi, kwa ajili ya wananchi wake waliomtuma kuhakikisha kwamba, tunamtua mama ndoo kichwani. Sisi Serikali tunaahidi kumpa ushirikiano mzuri kabisa kuhakikisha kwamba anatimiza azma yake ya kuwatumikia Wanakakonko.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu ambao Mheshimiwa Mbunge amesema, ni kweli kabisa Kijiji cha Kihomoka kina centre mbili. Centre ya kwanza tulichimba kisima, tukajenga miundombinu na tayari wanapata huduma nzuri kabisa, lakini Centre B ambayo ni kilometa 10 kuna wafugaji zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, kama nilivyojibu katika jibu la msingi, tunaiingiza kwenye programu ya vijiji 1,575 katika mwaka wa fedha 2026/2027, ili sasa tuchimbe kisima kwa kutumia mitambo ambayo Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alinunua katika mikoa yote 26. Itaenda kufanya hiyo kazi bila kuwa na changamoto yoyote na wananchi wa Kakonko watapata huduma ya majisafi na salama, hasa katika eneo la Kihomoka.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Ninampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa kulitazama suala la vitendea kazi. Vitendea kazi hivi vinasaidia sana watendaji wetu katika utekelezaji wa miradi, katika usimamizi wa miradi na katika shughuli mbalimbali za kiofisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunatambua umuhimu huu na Mheshimiwa Mbunge amefika mpaka kwa Mheshimiwa Waziri na ameongelea kuhusu hili suala. Ninataka nimpe Mheshimiwa Mbunge habari njema, kwamba Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ametupatia fedha kwa ajili ya kununua magari 29 mapya ili kwenda kuwasaidia watendaji wetu kutekeleza majukumu yao. Ninamtoa hofu DM wa Kakonko, yupo kwenye orodha hiyo ya kupatiwa gari, ili aweze kusimamia miradi vizuri na iwe na tija kwa wananchi.

Name

Mwamengo Ulimboka Baraka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyela

Primary Question

MHE. ALAN T. MVANO aliuliza: - Je, lini Mkandarasi atakamilisha kuchimba na kujenga kisima cha maji katika Kijiji cha Kihomoka kama ilivyo kwenye mkataba wake?

Supplementary Question 2

MHE. BARAKA A. U. MWAMENGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa Miradi ya Angana Group, Miradi ya Mbambo Group ndani ya Jimbo la Kyala ambayo imekwama kwa muda mrefu wakandarasi hawajalipwa?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninamtoa hofu Mheshimiwa Mbunge, tunao mpango, tumepanga vipaumbele na miradi ambayo ipo katika utekelezaji tunayo. Tunayo maelekezo ya kuhakikisha kwamba, tunakamilisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunamhakikishia Mheshimiwa Mbunge tutaongeza nguvu ya kupeleka fedha ili wakandarasi warudi, ambao wamekuwa wanasuasua, waweze kuongeza speed ya utekelezaji wa miradi hiyo, ili iweze kukamilika na wananchi waweze kupata huduma ya majisafi na salama.

Name

Edward Olelekaita Kisau

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiteto

Primary Question

MHE. ALAN T. MVANO aliuliza: - Je, lini Mkandarasi atakamilisha kuchimba na kujenga kisima cha maji katika Kijiji cha Kihomoka kama ilivyo kwenye mkataba wake?

Supplementary Question 3

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, wakati wa ziara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, tumewaeleza Vijiji 12 vya Kiteto ambavyo havina majisafi na salama. Ninajua bajeti yetu inakuja, sasa ni nini kauli ya Serikali kwa Vijiji 12 vya Kiteto ambavyo havina maji?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nimejibu katika majibu mengine kuhusiana na vijiji katika vijiji 12,318 nchi nzima, tunavyo vijiji 1,575 tu vilivyobaki. Hivi vijiji 1,575 tunaweka programu maalum ya utekelezaji kwa miaka mitano.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawahakikishia Waheshimiwa Wabunge, hivi vijiji 1,575 tumevigawa kwa awamu na kila awamu itagusa kila jimbo na kila mkoa kuhakikisha kwamba, tunaendelea kutekeleza awamu kwa awamu, lakini kila jimbo linakuwa linaguswa kila awamu, ambayo tunakuwa tunaitekeleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninamtoa hofu Mheshimiwa Mbunge, vijiji hivyo 12 tutavigawa kwa awamu, kama viko 12, basi tutaviweka viwili vitatu kila awamu, mwaka wa fedha, tunapokamilisha tunaingia awamu nyingine. Tuna uhakika itakapofika mwaka 2030 vijiji vyote 1,575 kuweka total ya 12,318 vitakuwa vimekamilika.