Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Juma Ramadhani Mustafa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igalula

Primary Question

MHE. JUMA M. KAWAMBA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza Shule za Msingi na Sekondari, pamoja na miundombinu katika Shule zilizopo Jimbo la Igalula?

Supplementary Question 1

MHE. JUMA M. KAWAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Jimbo la Igalula linapatikana maeneo ya kijijini ndani ya Mkoa wa Tabora, lakini tuna shule shikizi takribani 35 ambazo zimejengwa kwa nguvu za wananchi. Je, Serikali ina mkakati gani sasa wa kuleta fedha kwa ajili ya kumalizia shule hizi ndani ya Jimbo la Igalula?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Serikali ina mkakati gani wa kutuletea fedha kwa ajili ya kumalizia na kujenga shule za sekondari zifuatazo; Shule ya Sekondari Ipululu iliyopo Kata ya Igalula, Shule ya Sekondari Malakaseko iliyopo Kata ya Goweko, Shule ya Sekondari Itona iliyopo Kata ya Loya na Shule ya Sekondari ya Uyui Modern School? Hii ni shule ya amali iliyopo katika Kata ya Goweko, ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza, ninawapongeza sana wananchi wa Jimbo la Igalula kwa kuanza ujenzi wa shule za msingi shikizi 35. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali inatambua juhudi hizo za wananchi na itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kwenda kumalizia ujenzi wa shule hizi kwa awamu ili ziweze kutoa huduma ya elimu kwa watoto wetu. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, tunazitambua shule hizi na tunaendelea na taratibu za kupata fedha, ili kuendelea kuzikamilisha kwa awamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikijibu swali la pili, tunafahamu ziko shule ambazo zimejengwa, lakini hazijakamilika ikiwemo hii Shule ya Igalula Modern na nyingine zote ambazo Mheshimiwa Mbunge umezitaja. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mpango ambao tunaendeleanao, ukiwemo mpango wa kuanza naye double cohort ya Januari, 2028, yako maeneo ambayo tumeshayafanyia tathmini. Tutapeleka fedha kwa ajili ya kukamilisha shule ambazo zipo, lakini yako maeneo ambayo tutajenga shule nyingine kwa hiyo, katika kipindi hicho tutahakikisha tunatoa kipaumbele katika shule ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaja.

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JUMA M. KAWAMBA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza Shule za Msingi na Sekondari, pamoja na miundombinu katika Shule zilizopo Jimbo la Igalula?

Supplementary Question 2

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Je, Serikali imejipangaje kwa nchi nzima kukamilisha nyumba za walimu ambazo hazijakamilika, madarasa ambayo hayajakamilika na maabara ambazo hazijakamilika kwa nchi nzima?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba, tunazo nyumba za walimu, maabara, madarasa na baadhi ya miundombinu ya elimu ambayo shughuli za ujenzi zimeanza na zinaendelea katika hatua mbalimbali lakini hazijakamilishwa. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Cecilia Paresso kwamba, Serikali inatambua umuhimu wa kukamilisha miundombinu hiyo, na tayari kwenye bajeti zetu hata bajeti ijayo ya 2026/2027 tumetenga fedha kwa ajili ya kukamilisha miundombinu hiyo. Pia tutaendelea kutenga fedha kuhakikisha miundombinu hiyo inakamilika na kutoa huduma ambayo inatakiwa.

Name

Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songea Mjini

Primary Question

MHE. JUMA M. KAWAMBA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza Shule za Msingi na Sekondari, pamoja na miundombinu katika Shule zilizopo Jimbo la Igalula?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. DAMAS D. NDUMBARO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Kata ya Seed Farm, Manispaa ya Songea, haina sekondari ya kata. Je, ni lini Serikali itajenga sekondari ya kata katika kata hiyo ya Seed Farm?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge wa Songea Mjini, kaka yangu Ndumbaro, amefuatilia mara kadhaa suala la ujenzi wa shule ya sekondari katika Kata ya Seed Farm, Manispaa ya Songea. Ninaomba nimhakikishie tu kwamba, tuko hatua za mwisho. Tulikubaliana na wataalamu wafanye tathmini ya vigezo na baada ya hapo tuhakikishe tunapeleka fedha, kwa ajili ya kuanza ujenzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutahakikisha baada ya kupokea vigezo hivyo na kufanya tathmini, tutatoa kipaumbele kinachotakiwa kupitia mapato ya ndani ya Manispaa ya Songea na Serikali Kuu, ili tuweze kujenga shule hiyo ikiwa vigezo vitakuwa vimefikiwa.

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. JUMA M. KAWAMBA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza Shule za Msingi na Sekondari, pamoja na miundombinu katika Shule zilizopo Jimbo la Igalula?

Supplementary Question 4

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Makete bado tuna uhitaji wa sekondari, hususan kwenye Kata ya Mlondwe, ambayo hata Mheshimiwa Waziri anaifahamu; kama wilaya na kama halmashauri tumeandaa eneo. Ni lini Serikali itatoa fedha kwenye kipaumbele hiki cha wananchi wa Wilaya ya Makete ili Shule ya Sekondari Mlondwe ijengwe?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ninamhakikishia Mheshimiwa Festo Sanga, Mbunge wa Makete, kwamba Serikali inatambua umuhimu wa kujenga shule za sekondari katika kata ambazo hazina sekondari, kama Kata ya Bulongwa na hivyo tutahakikisha tunaweka vipaumbele. Jambo la msingi tunafanya tathmini ya vigezo, tukijiridhisha tutahakikisha tunapeleka shule kwa ajili ya kusogeza huduma za elimu karibu na wananchi.

Name

Neema Peter Majule

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JUMA M. KAWAMBA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza Shule za Msingi na Sekondari, pamoja na miundombinu katika Shule zilizopo Jimbo la Igalula?

Supplementary Question 5

MHE. DKT. NEEMA P. MAJULE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kuuliza, je, Serikali ipo tayari kubaini yale maeneo ya shule ya msingi ambayo ni makubwa, ambayo yana uwezo wa kujengwa sekondari palepale ili kuendana na huu mpango wa elimu jumuishi, yaani shule ya msingi na palepale sekondari?

Mheshimiwa Naibu Spika, samahani; kwa mfano hapa Dodoma, Shule ya Ipagala 'A' ina eneo kubwa sana ambalo hapo hapo ingeweza kujengwa sekondari, ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya Mheshimiwa Dkt. Neema ni ya msingi, na Serikali tayari imeanza. Yako maeneo ambayo yana shule za msingi zenye maeneo makubwa, maeneo hayo pia, yametumika kujenga shule za sekondari. Kwa hiyo, zoezi hili tutaendelea kulifanya. Tutapita pia, kwenye Shule ya Msingi ya Ipagala 'A', kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge, ili tuweze kuona kama kuna uhitaji wa ujenzi wa shule ya sekondari na kama eneo linatosha, basi Serikali itaendelea kuyafanyia kazi.

Name

Haiderali Hussein Gulamali

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ilongero

Primary Question

MHE. JUMA M. KAWAMBA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza Shule za Msingi na Sekondari, pamoja na miundombinu katika Shule zilizopo Jimbo la Igalula?

Supplementary Question 6

MHE. HAIDERALI H. GULAMALI: Mheshimiwa Naibu Spika, tumkumbushe Mheshimiwa Waziri kwamba, pale Ilongero shule zetu zina uchakavu mkubwa sana, zinatakiwa ukarabati katika kata mbalimbali. Tuliwasilisha maombi yetu kwa maandishi ofisini kwa Mheshimiwa Waziri. Tunaomba majibu.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninawapongeza wananchi wa Jimbo la Ilongero pamoja na Mheshimiwa Mbunge kwa kuwasilisha orodha ya shule ambazo ni chakavu na zinahitaji ukarabati. Ninaomba nimhakikishie kwamba, Serikali inaandaa mpango mkakati mahususi ambao utaainisha shule zote chakavu ambazo tayari, of course tumeainisha, lakini tunatafuta fedha kwa ajili ya kuona namna ambavyo tutakwenda kuzikarabati shule zile kwa awamu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie kwamba katika vipaumbele ambavyo vipo kwenye sekta ya elimu ni pamoja na kwenda kuondokana na shule chakavu na kongwe. Tunaendelea na taratibu za kupata fedha, ili tuje kukarabati. Tutahakikisha kwamba shule za Jimbo la Ilongero pia zitapata kipaumbele.