Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Eng. Johnston Johansen Mutasingwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Mjini
Primary Question
MHE. ENG. JOHNSTON J. MUTASINGWA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha upanuzi wa Kituo cha umeme Kibeta?
Supplementary Question 1
MHE. ENG. JOHNSTON J. MUTASINGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda niishukuru Serikali kwa majibu mazuri iliyoyatoa na sasa naona changamoto ya umeme kupungua au low voltage katika Jimbo letu la Bukoba Mjini linaenda kutoweka. Sasa ninapenda kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Je, ni lini Serikali sasa itamlipa huyu mkandarasi ili aweze kumaliza hiyo kazi kwa wakati na kama Serikali ilivyoahidi?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, katika Jimbo letu la Bukoba Mjini tuna Kata kama nane ambazo zinapakana na Jimbo la Bukoba Vijijini ambazo ni Ijuganyondo, Tendagulo, Kibeta, Kashai hasa maeneo ya Rwomwe, Ijuganyondo, Kahororo na Buhembe. Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia wananchi hawa umeme wa REA kwa shilingi 27,000 ili waweze na wenyewe kupata huduma ya umeme kwa uhakika, ahsante. (Makofi)
Name
Steven Lemomo Kiruswa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Longido
Answer
NAIBU WAZIRI WA MADINI K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninaomba kumpongeza Engineer Mutasingwa, Mbunge wa Bukoba Mjini kwa jinsi ambavyo amekuwa mtetezi wa dhati wa mahitaji ya msingi ya wapigakura wake wa Jimbo la Bukoba Mjini. Engineer huyu kwa kweli anapenda wapigakura wake wajue kwamba hawakukosea kumleta katika Bunge lako Tukufu, maana ni mtetezi wa kweli wa mahitaji ya watu wake. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la msingi, ni lini huu mradi utakamilishwa wa kuongeza hiyo transfoma ya kuongeza umeme ambao umeshatekelezwa kwa 65%, ninapenda kukuhakikishia kwamba, kwa kuwa IPT imeshapelekwa Wizara ya Fedha, mkandarasi huyu atalipwa na mradi huu unakwenda kukamilika ndani ya muda uliopangwa ambao ni kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili kuhusu Kata na Vijiji alivyovitaja anavyoviombea vipewe umeme wa REA, hizi bila shaka ni vile vijiji vinavyopakana na Miji, tunaviita Peri-urban areas ambavyo kuna siku Waziri amesimama hapa katika Bunge lako Tukufu akatoa ufafanuzi kwamba vijiji hivyo vinavyopakana na miji yenye hadhi ya vijiji, vyote vitakwenda kupatiwa umeme wa REA kwa bei ya shilingi 27,000. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Deodatus Philip Mwanyika
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Njombe Mjini
Primary Question
MHE. ENG. JOHNSTON J. MUTASINGWA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha upanuzi wa Kituo cha umeme Kibeta?
Supplementary Question 2
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi. Halmashauri ya Mji Njombe ni eneo linalokua kiuwekezaji, lakini haliwezi kuendelea na kupata wawekezaji wengi kama hatuna substation. Ni lini Serikali itajenga substation kubwa itakayovutia uwekezaji Njombe? (Makofi)
Name
Steven Lemomo Kiruswa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Longido
Answer
NAIBU WAZIRI WA MADINI K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara ya Nishati, imeshafanya tathmini ya mahitaji ya umeme katika nchi nzima na ni katika azma hiyo Serikali imeweza kufikisha umeme katika vijiji vyote vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na maeneo yote yanayohitaji kuongezewa nguvu ya umeme, transfoma, na vituo vya kupoza umeme. Pia vinazingatia ikiwa ni pamoja na eneo lake. Kwa hiyo, nimhakikishie kwamba Serikali ipo kazini kuhakikisha kwamba atafikishiwa umeme wanaouhitaji.
Name
Japhael Masanja Lufungija
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ulyankulu
Primary Question
MHE. ENG. JOHNSTON J. MUTASINGWA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha upanuzi wa Kituo cha umeme Kibeta?
Supplementary Question 3
MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana kwa nafasi hii. Jimbo la Ulyankulu ni miongoni mwa majimbo yenye shida kubwa ya kukatikakatika kwa umeme mara kwa mara, na wakati huo huo umeme tunaupata kutoka Mkoani Tabora zaidi ya kilometa 90, na tunayo miradi mingi ya uwekezaji ikiwepo migodi ya madini, vituo vya afya sita na sekondari...
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa umezima, washa kisemeo.
MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itatujengea switching station kwa ajili ya kuweka uimara ya ukatikaji wa umeme katikaJimbo la Ulyankulu?
Name
Steven Lemomo Kiruswa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Longido
Answer
NAIBU WAZIRI WA MADINI K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninampongeza Mheshimiwa Mbunge pia kwa maswali hayo mazuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaendelea kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu kwamba mpango wa Serikali wa kusambaza umeme toshelevu katika maeneo yote ya nchi yetu unaendelea. Baada ya ukamilishaji wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, sasa hivi shida ya nchi yetu siyo umeme tena, ni ujenzi wa miundombinu ya kufikisha umeme kwa walengwa wote ikiwepo migodi, sehemu za kutoa huduma za afya kama elimu na maeneo yote ya matumizi ya jamii na hasa maeneo ya biashara ambayo inaiingizia Taifa mapato.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge, awe na subira, utekelezaji wa miradi yote inaendelea sambamba na sawia katika nchi nzima ikiwepo eneo lake.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved