Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Esther Nicholas Matiko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Tarime Mjini
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza: - Je, lini Mradi wa Maji Ziwa Victoria utakamilika na kutoa huduma ya Maji kwa Mitaa yote 81 ndani ya Mji wa Tarime?
Supplementary Question 1
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana. Mradi huu ulitarajiwa kukamilika Novemba, 2025, wakafanya extension kuja Septemba, 2026. Nimeuliza takribani mara 40. Bunge lililopita niliuliza takribani mara 26 na Bunge hili takribani mara 10.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa, kwa kuwa Mji wa Tarime una mitaa 81 una kata nane. Kata nne tu ndizo zinapata kama takribani 45% za maji; kata nne nyingine hazipati kabisa maji; na zile kata zina mitaa, lakini zina taswira kama ya vijiji. Ninataka kujua ni kwa nini sasa Serikali iweke mpango wa dharura wakati tukisubiri mradi huu ambao unachukua muda mrefu sana?
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ione kuwa kuna haja ya kuchimba visima kwenye kata hizi, ili hii mitaa ambayo haina maji kabisa, hasa kwenye taasisi za shule na vituo vya afya waweze kupata maji wakati tukisubiria huu mradi wa Ziwa Victoria kama vile ambavyo wenzenu wa umeme wanafanya wanapeleka REA kwenye mitaa hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, mradi huu wakati unapita, kuna wananchi ambao ardhi zao zimechukuliwa kwa ajili ya kupisha mradi huu lakini mpaka sasa wananchi hawa hawajajua hatma yao lini watalipwa fidia zao. Ninataka nijue ni mkakati gani Serikali ilionao wa haraka kuhakikisha kwamba wanawalipa wale wananchi fidia waliopisha mradi huu ili kuendelea kupata baraka wakati wanajenga mradi huu?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Esther Matiko kwa kazi kubwa ambayo ameendelea kuifanya ya kuwasemea wana Tarime Mjini. Pia ninakiri, ukiachana na Bunge lililopita ndani ya kipindi hiki cha Bunge, nimejibu hili swali la Mheshimiwa Esther Matiko zaidi ya mara 10, ninatambua kabisa.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunatambua kwamba mradi huu una maslahi makubwa sana kwa Majimbo ya Tarime Mjini, Tarime Vijijini, na Rorya; na Waheshimiwa Wabunge wote, akiwemo Mheshimiwa Waitara pamoja na Mheshimiwa Chege wamekuwa wakiuongelea mradi huu. Sisi kama Serikali tumesikia sauti ya Wanatarime, tumesikia sauti ya wananchi wake na sisi tutahakikisha kwamba tunaongeza speed ya kupeleka fedha ili mradi huu uende kwa kasi zaidi ili uweze kutoa matokeo kwa haraka.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na fidia, labda niseme hivi, kuhusu fidia ya wananchi tulikubaliana na wananchi wake. Sehemu ambapo bomba linapita Serikali haitalipa fidia, tulikubaliana na kwa maandishi. Maeneo ambayo tunalipa fidia ni eneo la chanzo cha maji, eneo la booster station na eneo la mtambo wa kutibu maji; na katika eneo hilo tayari tumeshalipa zaidi ya milioni 36. Orodha tunayo, Mheshimiwa Mbunge akiomba tutampatia.
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile tunatambua kwamba tuna zaidi ya wananchi 20 ambao wameshalipwa. Eneo ambapo bomba linapita hatulipi fidia ya ardhi, tunalipa fidia ya uharibifu wa mazao. Tayari tumeshafanya tathmini, tunahitaji shilingi milioni 40 na tayari malipo yanaendelea. Kwa hiyo, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, tuko makini kuhakikisha kwamba wananchi wake wanapata haki yao kulingana na jinsi ambavyo wamejitolea ili mradi huu uweze kupita.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu hivi vijiji katika kata ambazo Mheshimiwa Mbunge amesema, kata hizi changamoto yake kubwa ni kwamba, visima vinapochimbwa katika hizi kata baada ya kuweka pampu, maji yanakauka. Pia tatizo kubwa la Tarime Mjini vyanzo vya maji ni shida.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninafahamu kwamba umuhimu wa wananchi katika kata hizi tano ikiwemo Nyandoto, Nankende. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba hizi kata tumemwelekeza MD aweze kufanya tathmini, iwapo katika kata nyingine kuna mradi ambao una maji ya kutosha, tufanye extension kwenda katika hizo kata ambazo zina changamoto ya maji wakati tukiwa tunasubiri utekelezaji wa mradi mkubwa wa Ziwa Victoria wa shilingi bilioni 134 ambao ni uwekezaji mkubwa sana wa Serikali ya Awamu ya Sita. Ninakushukuru sana.
Name
Kunti Yusuph Majala
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza: - Je, lini Mradi wa Maji Ziwa Victoria utakamilika na kutoa huduma ya Maji kwa Mitaa yote 81 ndani ya Mji wa Tarime?
Supplementary Question 2
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa kunipatia nafasi ili nami niweze kumwuliza Mheshimiwa Naibu Waziri swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Kelemasimba ambao upo Kata ya Dalai, na Mradi wa Ovada wa Kata ya Ovada, na Mradi wa Maji wa Kubunko ulioko Kata ya Makorongo, miradi hii imekuwa ya muda mrefu, ina takribani zaidi ya miaka miwili haijakamilika. Je, kuna mkakati gani wa haraka wa kukamilisha miradi hii ili wananchi wangu wa Wilaya ya Chemba waweze kupata maji?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kumshukuru sana Mheshimiwa Mbunge ambaye pia anatoa ushauri na taarifa, na anawasemea wananchi wa Chemba. Sisi Serikali, dhamira yetu ni kuhakikisha kwamba miradi inakamilika. Nimtoe hofu, tutaongeza speed ya kupeleka fedha katika kata hizo ili mkandarasi aweze kukamilisha miradi hiyo na wananchi wake waweze kupata huduma ya majisafi na salama.
Name
Dr. Regina Christopher Malima
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza: - Je, lini Mradi wa Maji Ziwa Victoria utakamilika na kutoa huduma ya Maji kwa Mitaa yote 81 ndani ya Mji wa Tarime?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. REGINA C. MALIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa kunipatia nafasi. Ni jambo la kushangaza kuwa wananchi wa Kisiwa cha Ukerewe kinachozungukwa na Ziwa Victoria hawana majisafi na salama, ikiwemo Kijiji cha Busagami Kata ya Namilembe. Nini kauli ya Serikali juu ya hali hii, na ni hatua gani za haraka zitachukuliwa kuhakikisha wananchi wa kisiwa hiki wanapata huduma ya majisafi na salama?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninafahamu kwamba kiu ya Mheshimiwa Mbunge ni kuhakikisha wananchi wake wa Ukerewe wanapata huduma ya majisafi na salama kwa 100%, lakini mpaka sasa upatikanaji wa maji ndani ya Kisiwa cha Ukerewe ni zaidi ya 65%.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunaamini kwamba kiu yake ni kwamba tuongeze ili wananchi wengi zaidi wakiwemo katika Kijiji ambacho Mheshimiwa amekitaja, nikuhakikishie Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza, tayari wanafanya tathmini ya kujua ukubwa wa tatizo ili waweze kufanya usanifu na tuweze ku-establish gharama za kwenda kutekeleza miradi ambayo itatatua changamoto ya maji katika Jimbo la Ukerewe. Ninakushukuru sana.
Name
Paschal Inyasi Chinyele
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Dodoma mjini
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza: - Je, lini Mradi wa Maji Ziwa Victoria utakamilika na kutoa huduma ya Maji kwa Mitaa yote 81 ndani ya Mji wa Tarime?
Supplementary Question 4
MHE. PASCHAL I. CHINYELE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Wakazi wa Mitaa ya Kata za Chang’ombe, Nkuhungu, Mnadani pamoja na Nala, wanakabiliwa na uhaba mkubwa sana wa maji. Hii ni kutokana na kuzidiwa kwa Mfumo wa Maji wa Mzakwe. Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa miradi ya maji ya Nzuguni, Nala pamoja na Zuzu ili kuepusha uhaba huo wa maji? Katika kata hizi, vipo vituo vya afya kama Chang’ombe pamoja na Zuzu, lakini havina maji. Ni lini Serikali itashughulikia tatizo hilo?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge wa Jiji la Dodoma ambapo nikiri kabisa kwamba hata ofisini kwetu ameshakuja mara kadhaa, ili kuendelea kuwasemea wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini, wakiwemo Wabunge wanaoishi katika Jiji la Dodoma. Mheshimiwa Chinyele, kwenye suala la miradi yetu, tunao mradi wa Nzuguni, Serikali imewekeza zaidi ya shilingi 9,000,000,000.
Mheshimiwa Naibu Spika, Nzuguni One ambapo mradi huo umefikia 98% bado tu kidogo ukamilike. Pia tuna Nzuguni Two ambao unaendelea. Tuna mradi wa Nala ambao pia Serikali imewekeza shilingi 4,000,000,000, tunao Mradi wa Zuzu ambao tumeweka shilingi 7,000,000,000 ambapo kwa ujumla wake huo, mahitaji ya Jiji la Dodoma ni lita 160,000,000 mpaka sasa uzalishaji wetu ni lita 80,000,000.
Mheshimiwa Naibu Spika, miradi hii mitatu yote itakapokamilika tutaongeza uzalishaji wa maji kutoka lita 80,000,000 mpaka lita 120,000,000. Maana yake ni kwamba tutakuwa tumefikia zaidi ya 80% ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Jiji la Dodoma.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inaendelea na michakato ya miradi hii, na ipo katika hatua nzuri kabisa. Miradi hii itakapokamilika wananchi wa Jiji la Dodoma pamoja na Jimbo la Mtumba itakuwa ina uhakika wa kupata majisafi na salama, wakiwemo Wabunge wanaoishi katika Jiji hili la Dodoma.