Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Timida Mpoki Fyandomo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TIMIDA M. FYANDOMO K.n.y. MHE. DICKSON N. LUTEVELE aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuondoa Kodi ya 30% katika export ya Mazao ya Misitu ambayo imeua kabisa Viwanda?

Supplementary Question 1

MHE. TIMIDA M. FYANDOMO: Mheshimiwa Mwenyekiti nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Tangu kuanzishwa kwa kodi hii, idadi ya kontena za vinea ambazo zimekuwa zikisafirishwa zimepungua kutoka kontena 3,765 mpaka kontena 2,110 mwaka 2026 hadi mwezi huu Machi. Je, Serikali imefanya tathmini ya kulinganisha mapato inayopata kupitia kodi hii dhidi ya ajira zilizopotea kwenye viwanda vya misitu?

Name

Amb. Khamis Mussa Omar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba kunakuwa kuna haja ya kufanya tathmini kwenye athari ambazo zimetokeza kutokana na hatua hizi. Hata hivyo, kama nilivyoeleza katika jibu langu la msingi, dhamira moja ya hatua hii ilikuwa ni kupunguza usafirishaji nje ya nchi. Kwa hiyo, kutokana na alichokisema Mheshimiwa Mbunge, inaonekana kweli upande mmoja tumefanikiwa, lakini upande wa pili tunahitaji kufanya tathmini kuona sasa zile faida ambazo zilitarajiwa kama zimepatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kama ambavyo imesemwa hatua hii ilianza kutekelezwa mwezi Julai, 2025, vipindi ni vifupi kufanya tathmini. Tunalipokea na kwamba tutafanya tathmini kama nilivyosema awali, sisi kwa ushirikiano na Wizara ya Utalii na Maliasili.