Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ester Edwin Malleko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza skimu za umwagiliaji katika Mkoa wa Kilimanjaro?
Supplementary Question 1
MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina swali moja la nyongeza. Kwa kuwa baadhi ya miradi iko kwenye wastani wa 28% na 45%, je, ni upi mkakati wa Serikali sasa kuhakikisha miradi hii inatekelezwa kwa kasi ili wananchi waweze kufaidika mapema?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza Mheshimiwa Esther Maleko kwa swali zuri la msingi na kufuatilia wananchi wake wa mkoa mzima wa Kilimanjaro. Jambo moja ambalo ninaweza nikamthibitishia kwa 100% ni kwamba miradi hii itakamilika kama ambavyo imepangwa. Kwa kuwa Wizara ya Fedha, sasa hivi ilishaweka commitment ya kuipatia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kila mwezi shilingi bilioni 25 zitakazokwenda kwenye miradi ya umwagiliaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, fedha hizo zitasaidia kusukuma hii miradi iweze kukamilika kwa wakati kwa sababu tutawalipa kwa wakati, na sisi tutawasimamia kuhakikisha miradi hii inaenda kwa kasi. Kwa hiyo, nimwondoe shaka Mheshimiwa Mbunge kwamba na sisi tuko katika area of comfort kwamba miradi hii inakwenda kukamilika, ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved