Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa minara ya mawasiliano Halmashauri ya Mji Ifakara hasa Ikwambi, Mang’ula B na Kanyenja?

Supplementary Question 1

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na ninaishukuru Serikali kwa majibu mazuri na timu ya watu wa Wizara walifika jimboni kwangu, wakatembelea maeneo yote ambayo tuliomba minara. Tuliomba minara 10 na tumepewa minara nane, ni imani yangu kama majibu ya Serikali yalivyo, katika minara miwili ya Ikwambi na Mang'ula B basi itaanza kujengwa haraka iwezekanavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Swali la kwanza, katika minara hii nane ambayo tumeipata kuna tatizo la changamoto la usikivu mdogo, kwa mfano pale Lumemo, Ihanga kuna mnara lakini bado kuna changamoto ya mawasiliano. Je, ni lini mpango wa Serikali kupitia katika minara ambayo imejengwa ili sasa kuiongezea nguvu iweze kusikika vizuri kwa maana ya 2G iende kwenye 4G?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ni lini mpango wa Serikali wa mnara mmoja kutumika na kampuni zote utaanza, kama ambavyo Kamati ya Bunge tumeshauri? Sehemu ambako Tigo wamejenga tusianze kuhangaika kutafuta tena wengine wakajenge. Ninakushukuru.

Name

Switbert Zacharia Mkama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kumpongeza Mheshimiwa Asenga ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati inayosimamia Wizara yetu. Amekuwa mtu hodari katika Kamati, mchangiaji mzuri na mshauri mzuri, hakika wananchi wa Kilombero wamepata Mbunge jembe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nininaomba nijibu maswali yake mawili ya nyongeza kama ifuatavyo; kuhusu minara iliyojengwa kwake kuwa na nguvu kidogo, hili tatizo huwa linatokea kutokana na inapojengwa baadaye watumiaji wanaongezeka na makazi yanaongezeka. Kwa hiyo, nguvu inapungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia Bunge lako Tukufu ninamwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa TCRA kuifanyia tathmini minara hiyo, kugundua udhaifu uliopo na kuwasiliana na watoa huduma walioijenga hiyo minara ili waweze kuiongezea nguvu kulingana na tathmini itakayofanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili, Serikali inaendelea na mkakati wake wa kujenga minara kupitia mkakati wa miaka mitano. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika maeneo yote ambayo tumeyagundua kwamba yana changamoto ya mawasiliano katika eneo lake tutayaingiza katika mpango wa Wizara wa ujenzi wa minara kwa mwaka ujao wa fedha wa 2026/2027. Ninakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la mnara mmoja kutumiwa na watoa huduma wengi au roaming, tunaendelea na mazungumzo, TCRA inafanya mazungumzo na watoa huduma ili kuwezesha huduma hii kwamba mnara mmoja unatumiwa na watoa huduma wengi. Baadhi ya mashirika kama...

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa, wewe zima hiyo.

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, TTCL na Airtel wameshaanza hiyo huduma. Tunaendelea kufanya mazungumzo na watoa huduma wengine ili hili liwezekane kwamba mnara mmoja kutumiwa na watoa huduma wengi.

Kwa hiyo, nitumie nafasi hii pia kupitia Bunge lako Tukufu kumwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa TCRA kuharakisha hayo mazungumzo ili mpango huu uanze kutekelezwa.

Name

Mohamed Mussa Utaly

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lindi Mjini

Primary Question

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa minara ya mawasiliano Halmashauri ya Mji Ifakara hasa Ikwambi, Mang’ula B na Kanyenja?

Supplementary Question 2

MHE. MOHAMED M. UTALY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, niwashukuru sana wizara hii kwa kutupatia mnara katika Kata ya Tandangongoro. Tandangongoro sasa inazungumza; je, ni lini Serikali itajenga minara ya mawasiliano katika Jimbo la Lindi, hususan katika maeneo ya Kata ya Chikonji, Kitumbikwela, Mbanja na Rasbura?

Name

Switbert Zacharia Mkama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Lindi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wizara yetu tunatekeleza mpango wa miaka mitano wa kujenga minara katika mikoa na wilaya zote nchini ikiwemo Jimbo la Lindi. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mpango wetu huu tutafika katika jimbo lake na tutafanya kama anavyoomba kujenga minara ya mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii pia kumwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa UCSAF kutuma wataalamu katika jimbo hili kufanya tathmini ya uhitaji wa minara katika jimbo lake ili tuingize katika mpango wetu wa miaka mitano wa ujenzi wa minara nchi nzima. Nakushukuru.

Name

Neema William Mgaya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa minara ya mawasiliano Halmashauri ya Mji Ifakara hasa Ikwambi, Mang’ula B na Kanyenja?

Supplementary Question 3

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kumekuwa na changamoto sana ya mtandao maeneo ya Kiumba, Kata ya Lyamkena Jimbo la Makambako lakini hali kadhalika Kata ya Ilembula Jimbo la Wanging'ombe kwenye baadhi ya vijiji kikiwemo na Igula.

Je, ni lini mtahakikisha kwamba mnaimarisha kwa kuweka minara ambayo wananchi hao waweze kupata mawasiliano vizuri bila usumbufu?

Name

Switbert Zacharia Mkama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nijibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Njombe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii kumwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa UCSAF kwenda katika Jimbo la Mheshimiwa Mbunge na Mkoa wa Njombe kufanya tathmini ya changamoto ya mawasiliano katika kata alizozitaja ili tutambue changamoto iliyopo na kupata namna bora ya kulitatua. Kama ni ujenzi wa minara mipya au kama ni kuongezea nguvu minara iliyopo basi tufahamu tutatumia njia gani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutakwenda katika jimbo lake na mkoa wake kufanya tathmini na pale tutakapogundua udhaifu tutarekebisha, kama ni ujenzi wa minara mipya tutajenga na kama ni kuongeza nguvu tutaongeza nguvu na katika mpango wetu wa miaka mitano tutahakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030 changamoto ya mawasiliano nchini tutakuwa tumeitatua kwa kiwango kikubwa kama siyo kuimaliza kabisa. Ninakushukuru.