Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwamengo Ulimboka Baraka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyela

Primary Question

MHE. BARAKA A. U. MWAMENGO aliuliza: - Je, lini Barabara ya Ipyana – Kasumulu – Ileje itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. BARAKA A. U. MWAMENGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa, eneo lile la Barabara hiyo ya Ipyana – Kasumulu kwa kipindi hiki cha mvua imeathirika sana na maeneo makubwa ambayo yanakwamisha magari kupita ni eneo hilo, hasa kipande cha eneo la Igoma, je, Serikali itakuwa tayari kupeleka fedha za dharura, ili kuendelea kuikarabati hiyo barabara wakati tunasubiri huo mradi mkubwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, kwa kuwa, Serikali tayari imesema kuwa, imeanza kipande, section ile ya upande wa Ileje, je, awamu ya pili itakuwa tayari sasa kuanza kipande cha Ipyana – Kasumulu – Ngana, ili wananchi waone Serikali inajali, kama ilivyoandikwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi? Ninashukuru. (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba, hii ni barabara ya changarawe, ambayo katika kipindi cha mvua na hasa ule Ukanda wa Kyela ambao una mvua nyingi, huwa barabara nyingi zinakuwa zimeharibika. Huu ni mwezi wa Tano, kwa hiyo, ninamwelekeza Meneja wa Mkoa wa Mbeya afike eneo la barabara kuangalia kama sasa tunaweza tukaanza utengenezaji wa kawaida, na kama sivyo, basi aweze kuhakikisha kwamba, mkandarasi ambaye atatengeneza barabara hiyo katika matengenezo ya kawaida, anatengeneza na kurekebisha yale maeneo ambayo sasa yanafanya hiyo barabara isipitike kwa urahisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili, barabara hii inaunganisha Mkoa wa Songwe na Mkoa wa Mbeya, kwa maana ya Wilaya ya Ileje na Wilaya ya Kyela. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, ombi la kuanza upande mwingine Serikali itasikiliza, lakini ninafahamu Mheshimiwa Mbunge pia ni mtaalamu wa barabara. Kuna vigezo kadhaa ambavyo vinaangaliwa, hasa kulingana na ushauri wa mhandisi mshauri, barabara ianze wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo barabara zinaanza katikati, nyingine zinaanza mwisho. Kwa hiyo, tutaangalia, kama kutakuwa na vigezo hivyo vya kuanza upande huo wa Ipyana, haitashindikana kufanya hivyo, ahsante. (Makofi)

Name

Anne Kilango Malecela

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Same Mashariki

Primary Question

MHE. BARAKA A. U. MWAMENGO aliuliza: - Je, lini Barabara ya Ipyana – Kasumulu – Ileje itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 2

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, kwa kuwa, Mheshimiwa Waziri alikuja Same tukapita Barabara ya Mwembe – Miamba – Ndungu, kwa siku nzima tulipitia barabara hii, sasa ninaomba kuuliza swali, je, ni lini barabara hii itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami? Ahsante. (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli nilipita hiyo barabara na ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, kwamba kwanza ni kweli hiyo barabara ilikuwa haijafanyiwa usanifu. Maana yake ilikuwa haijafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Ndiyo tupo kwenye hiyo kazi ya kufanya usanifu wa kina wa barabara hiyo, ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami, ahsante.

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. BARAKA A. U. MWAMENGO aliuliza: - Je, lini Barabara ya Ipyana – Kasumulu – Ileje itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 3

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muda mrefu sasa Serikali imetuahidi ukarabati wa Barabara ya Moshi – Arusha pamoja na kulipa fidia na kujenga Daraja la Kikafu. Serikali ina mpango gani sasa kuanza kutekeleza ahadi hii ambayo imekuwa ya muda mrefu?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii inatekelezwa kwa kutumia fedha ya Serikali ya Tanzania, lakini pia, ikisaidiana na wenzetu wa JICA. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa, mazungumzo yote yamekamilika, na no objection kwa maana ya kuwa na utayari wa kufanya hiyo kazi, imeshatolewa na wenzetu wa JICA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tupo kwenye hatua za mwisho kabisa ikiwa ni kutangaza hiyo kazi, kulipa fidia kwa wale watakaoathirika, lakini pia, na kujenga hilo Daraja la Kikafu ambalo tunalihamisha lilipokuwa na kuliweka sehemu nyingine, hasa kutokana na ukweli kwamba, daraja lililopo linaleta changamoto kubwa sana ya ajali. Kwa hiyo, tupo kenye hatua za mwisho kabisa.

Name

Aysharose Ndogholi Mattembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BARAKA A. U. MWAMENGO aliuliza: - Je, lini Barabara ya Ipyana – Kasumulu – Ileje itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 4

MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kuniona. Kwa kuwa, barabara inayoanzia Singida Mjini hadi Ilongero, kibali cha kujenga kilometa kumi zinazoanzia Mtipa kwenda Makao Makuu ya Jimbo la Ilongero kimetoka. Ninapenda kujua ni lini sasa Serikali itampata mkandarasi kwa ajili ya kujenga kilometa hizo kumi? Ninashukuru sana. (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hiyo ilikuwa imetangazwa, na mkandarasi alikuwa amepatikana mmoja, ambaye baada ya majadiliano ilionekana kwamba bei yake iko juu sana na hivyo kulazimisha barabara hiyo kutangazwa upya ili iweze kuwa ndani ya bajeti ambayo tunategemea barabara zetu zinajengwa kwa kiwango hicho, ahsante. (Makofi)