Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 1 2025-04-08

Name

Stella Simon Fiyao

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Mlowo – Isansa – Magamba hadi Mkwajuni Wilaya ya Songwe?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikipeleka fedha kwa ajili ya kuiboresha Barabara ya Mlowo – Isansa – Magamba hadi Mkwajuni ambapo katika mwaka 2019/2020, Serikali ilipeleka shilingi 294,630,000.00 kwa ajili ya kufungua barabara hii kipande chenye urefu wa kilomita 16.2 eneo la Magamba hadi Ilumbwe. Aidha, katika mwaka 2022/2023, Serikali ilitumia shilingi 75,684,400.00 kujenga Solid Drift safu mbili, box kalavati kubwa moja (two cells) na mifereji ya maji ya mvua mita 70.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile katika mwaka wa fedha 2022/2023 na 2023/2024, Serikali imetumia shilingi 365,395,000.00 kufanya matengenezo ya barabara kipande chenye urefu wa kilomita 13.1 kuanzia Mlowo hadi Isansa ambazo zimefanya kazi ya kuumba tuta la barabara kilometa 13.1, kuweka changarawe na kushindilia, kujenga safu saba za kalavati pamoja na kujenga mifereji ya maji ya mvua yenye urefu wa mita 1085.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuiboresha barabara hii kwa kuijenga na kuifanyia matengenezo mara kwa mara ili kuiimarisha zaidi kulingana na upatikanaji wa fedha.