Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Stella Simon Fiyao
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Mlowo – Isansa – Magamba hadi Mkwajuni Wilaya ya Songwe?
Supplementary Question 1
MHE. STELLA S. FIYAO: Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na umuhimu wa barabara hii wananchi wa Wilaya ya Songwe wamekuwa wakikutana na changamoto nyingi sana hasa wanapokuwa wanahitaji huduma makao makuu ya mkoa. Inawalazimu kupitia Mkoa mwingine wa Mbeya kabla ya kufika Makao Makuu ya Mkoa wa Songwe. Sasa, ninataka kujua ni lini Serikali itakamilisha barabara hii ili kuepusha adha ya gharama na muda kwa wananchi wa Wilaya ya Songwe?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu namba mbili, ninataka kujua ni lini watafanya marekebisho makubwa kwa kipande cha Barabara kutoka Isongole – Itumba Wilayani Ileje hasa ukizingatia kwamba barabara hii imebeba sura halisi ya makao makuu ya wilaya?  Ninashukuru sana. (Makofi)
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
								MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali zuri kabisa la Mheshimiwa Mbunge. Kwanza ninampongeza kwa nia yake thabiti ya kutaka kuwapambania wananchi ili waweze kupata barabara nzuri. (Makofi)  
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la kwanza la Mheshimiwa Mbunge kuhusiana na Barabara hii ya Mlowo – Isansa – Magamba kama nilivyotangulia kujibu kwenye majibu ya msingi, katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali ilitenga bajeti ya shilingi 344,650,000 kwa ajili ya kukarabati kipande cha kilomita 13.1. 
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, kutokana na umuhimu mkubwa wa barabara hii tayari mkoa kupitia kikao chake cha Bodi ya Barabara kilichoketi Machi 2024, umeomba idhini kwa ajili ya Barabara hii ya Mlowo – Isansa – Magamba kupandishwa hadhi kuwa miongoni mwa barabara zitakazohudumiwa na TANROADS.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili, Barabara hii ya Isongole – Itumba ni barabara ambayo inahudumiwa na TANROADS. Kwa hiyo, sisi kama Ofisi ya Rais, TAMISEMI, tutaendelea kuwasiliana na wenzetu wa Wizara ya Ujenzi ili kuhakikisha miundombinu hii inaweza kupatiwa fedha na kutengenezwa katika viwango ambavyo vitawanufaisha wananchi. (Makofi) 
							
 
											Name
Pauline Philipo Gekul
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Babati Mjini
Primary Question
MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Mlowo – Isansa – Magamba hadi Mkwajuni Wilaya ya Songwe?
Supplementary Question 2
MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Naibu Spika, barabara za Mji wa Babati zimeharibika sana, tangu mwaka jana TARURA hawajapewa fedha. Ni lini TARURA watapewa fedha ili watengeneze barabara hizo? Ninakushukuru. (Makofi)
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Gekul kwamba, Serikali ya Awamu ya Sita imefanya jitihada thabiti kabisa kwanza kuongeza bajeti ya TARURA kutoka shilingi bilioni 275 mpaka sasa kila mwaka TARURA ina bajeti ya shilingi bilioni 710. 
Mheshimiwa Naibu Spika, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya kuhakikisha barabara hizi za wilaya zenye umuhimu mkubwa sana kwa wananchi kiuchumi na kijamii zinaweza kujengwa na fedha zinatoka kila wakati.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge fedha zinaendelea kutoka na zitafika kwenye jimbo lake kwa ajili ya kuhudumia barabara hizi zenye umuhimu mkubwa sana kwa wananchi. (Makofi)
							
 
											Name
Dr. Christine Gabriel Ishengoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Mlowo – Isansa – Magamba hadi Mkwajuni Wilaya ya Songwe?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini Serikali itakarabati Barabara ya Mahenge – Mwaya – Ketaketa ambayo ni mbovu sana? Ahsante.
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu mkubwa sana wa barabara zetu hizi za wilaya ambazo zinawasaidia wananchi kiuchumi na kufikia huduma za kijamii. Serikali imekuwa ikitenga fedha kila mwaka kuhakikisha inazifikia hizi barabara, inaongeza mtandao mrefu zaidi wa barabara zenye hadhi ya juu zaidi ikiwemo hadhi ya lami. 
Mheshimiwa Naibu Spika, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, hata katika eneo hili alilolitaja Serikali itaendelea kuleta fedha kuhakikisha inakarabati na kujenga barabara hizi ili ziweze kuwanufaisha wananchi.
							
 
											Name
Hussein Nassor Amar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyang'hwale
Primary Question
MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Mlowo – Isansa – Magamba hadi Mkwajuni Wilaya ya Songwe?
Supplementary Question 4
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaanza kwa kuishukuru Serikali kwa kutujengea kilomita moja ya lami pale Makao Makuu Karumwa. Hata hivyo, barabara ile imejengwa na kunyanyuliwa juu na zile nyumba zilizoko pembezoni kuonekana kuwa chini. Mvua inaponyesha maji huingia kwenye nyumba za watu. Je, lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kujenga mifereji na kuzuia adha hiyo? (Makofi)
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimpongeze Mheshimiwa Mbunge Hussein Amar kwa kutaka kuona wananchi wake wanapata miundombinu mizuri ikiwemo mifereji kwa ajili ya kupokea maji ya mvua na kutokuleta adha kwa wananchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inafanya jitihada hizo na ndiyo maana kila mwaka inatenga fedha kwa ajili ya kukarabati barabara zetu hizi ambazo zinahudumiwa na TARURA. Serikali itafika katika eneo hili ili kuweza kujenga mifereji hiyo ili iweze kuwanufaisha wananchi. (Makofi)
							
 
											Name
Anne Kilango Malecela
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Same Mashariki
Primary Question
MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Mlowo – Isansa – Magamba hadi Mkwajuni Wilaya ya Songwe?
Supplementary Question 5
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi ninavyoongea hapa Barabara za Tarafa ya Mamba - Vunta na Gonja ambazo ni barabara za milimani zinazowafanya wananchi wateremke tambarare zote zimekufa. Je, lini Serikali itaziangalia hizi barabara kwa haraka ili wananchi wa milimani waweze kufikisha mazao yao kwenye masoko madogo na makubwa ambayo yako tambarare? Ninaomba jibu la uhakika. (Makofi)
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nianze kumpongeza Mheshimiwa Anne Kilango kwa swali lake zuri ambalo linalenga kuwaletea maendeleo wananchi wake. 
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie kwamba jitihada za Serikali zinafanyika kuhakikisha inafikia mtandao mkubwa zaidi wa barabara hizi zinazohudumiwa na TARURA ili kuweza kuwanufaisha wananchi. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali itafika katika tarafa hizi alizozitaja kwa ajili ya kuhakikisha inarekebisha barabara hizi, inazijenga katika kiwango ambacho hakitawakwamisha wananchi wako.